Home » » DR SLAA ALIVYOONYESHWA NGUVU YA ZITTO KIGOMA,WASEMA ZITTO KWANZA CHAMA BAADAE

DR SLAA ALIVYOONYESHWA NGUVU YA ZITTO KIGOMA,WASEMA ZITTO KWANZA CHAMA BAADAE

Hali ilivyo Mkoani Kigoma tangu jana wakati Dk Slaa akiendelea na ziara yake mkoani humo.
Taarifa hiyo inaeleza kwamba mikakati hiyo inalengo la kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa, ambaye leo anaendelea na ziara yake Mkoani humo,tangu Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazi kuvuliwa madaraka yake ndani ya Chama hicho, kufuatia madai ya kupanga njama za kuung'oa uongozi uliopo madarakani akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Slaa.
 Mikakati hiyo itafuatiwa na maandamano makubwa kueelekea eneo la mkutano, hii ni mara ya pili kwa mipango kama hiyo kufanyika baada ya ile ya jana kufanikiwa, ambapo mkutano wa Dk Slaa ulivunjika huku Askari wa Jeshi la Polisi wakilazimika kutumia nguvu na kurusha mabomu ya machozi kuwatanya wanachama wanaopinga ziara hiyo mkoani humo.
Wanachama wa Chadema wakichoma Bendela za Chama Mkoani Kigoma
Awali Uongozi wa Chadema Mkoa wa Kigoma ulitahadhalisha kuhusu ziara hiyo na kudai kwamba, hali si shwari katika mkoa huo kutokana na wanachama wa Chadema kuchoma Bendera na kubomoa mawe ya msingi katika ofisi mbalimbali za Chama hicho.
Wakati hayo yakiendelea Katibu Mkuu huyo (Dk Slaa) amekiri kuwepo kwa hali mbaya lakini akisisitiza kwamba, kamwe hawezi kukatisha ziara yake, mkoani humo na kama ikibidi kufa basi yuko tayari kufa, awali kabla ya vurugu hizo kuanza Habarimpya.com pia iliwai kuandika habari juu ya mikakati iliyopangwa na wanachama wa Chadema wanaopinga hatua ya Kamati Kuu ili kusoma habari hiyo bofya maandishi ya bluu.
Chanzo;Francis Godwin blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa