Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimeijia juu serikali kwa kumkumbatia mkandarasi
asiye na uwezo wa kujenga bandari ndogo ya Karema, mkoani Katavi.
CCM imewaomba radhi wananchi wa Karema na Mkoa wa Katavi kwa jumla
kutokana na madhara yanayosababishwa na kusimama kwa shughuli za
uzalishaji na usafirishaji kupitia bandari hiyo.
Bandari hiyo imechelewa kwa zaidi ya miaka mitatu kwa sababu ya serikali kumkumbatia mkandarasi huyo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha
Karema, Wilaya ya Karema, Mkoa wa Katavi, Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, alisema kitendo cha kuipa Kampuni ya Modispan kazi
nne za ujenzi wa gati ambayo haina uwezo wa kuifanya ni cha kihuni
kisichopaswa kufumbiwa macho.
Alisema serikali inapaswa kujieleza kwa nini mkandarasi huyo hadi leo
hajanyang’anywa ukandarasi wa kujenga bandari hiyo licha ya kutokuwa na
uwezo.
“Ndugu wananchi nakuombeni radhi kwa niaba ya CCM kutokana na kitendo
hiki cha hovyo ilichofanyika, hatupaswi kujifanya hatuoni wakati mambo
yako wazi kwa kazi kutofanyika.
“Yako maswali yanayopaswa kujibiwa kuhusu hiki kilichofanyika. Kwanza
ni nani aliyempa mkandarasi huyu kazi ya ujenzi bila kujiridhisha na
uwezo wake, pili kwa nini hadi sasa hajanyang’anywa kazi hii licha ya
kubainika ameshindwa,” alisema.
Kwa mujibu wa Kinana, amelichukua suala hilo ili likajadiliwe kwenye
vikao vya juu zaidi na kumtafuta mchawi ili hatua zaidi zichukuliwe.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment