Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI ya wanafunzi 450 wa shule nne za msingi katika Kata ya
Bumera, wilayani Tarime, watakosa masomo kwa muda usiojulikana kutokana
na vyumba vya madarasa wanavyovitumia pamoja na nyumba za walimu
kuezuliwa kwa upepo ulioambatana na mvua.
Mvua hiyo iliyonyesha Aprili 13, ilisababisha uharibifu katika shule
za Kwisarara, Taisi, Kitenga na Kiterere zilizoathirika kwa kiasi
kikubwa.
Katika Shule ya Msingi Kwisarara, vyumba viwili vya madarasa na ofisi
ya walimu vimebomolewa kuta zake, huku nyumba ya mwalimu mkuu
ikiezuliwa sehemu ya nyuma ya jengo hilo.
Akizungumzia athari hizo, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Roche Rajab,
alisema familia yake ilinusurika kifo kutokana na tufani iliyotangulia
nusu saa kabla ya mvua kuanza kunyesha, ikizifanya kuta za nyumba
kutikisika na kuwaogopesha watoto wake walioamua kukimbilia kabla ya
sehemu ya nyumba yake kung’olewa paa.
Shule ya Taisi yenye jumla ya wanafunzi 225, imelazimika kusimamisha
masomo kutokana na madarasa yao kubomoka na sehemu ya paa na choo
kuezuliwa na upepo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitenga, Kandoro Kasoga, alisema
amelazimika kulala katika nyumba ya wazi baada ya paa ya nyumba yake
kuezuliwa na upepo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment