Home » » AUA MGAMBO KULIPIZA KISASI

AUA MGAMBO KULIPIZA KISASI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
JESHI la Polisi mkoani hapa, linawashikilia Elias Balandese na Faustine Fidel kwa tuhuma za mauaji ya askari mgambo, Shabani Mbadi mkazi wa Kijiji cha Nyamidaho wilayani Kasulu kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali upande wa kushoto wa kifua chake.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema Mbadi alijeruhiwa Julai 24 mwaka huu majira ya saa nne usiku wakati wakinywa pombe za kienyeji pamoja na watuhumiwa.
Kashai, alisema kuwa Balandese ambaye ni raia wa Burundi, aliamua kulipiza kisasi kwa kumuua askari mgambo huyo kutokana na kumkamata katika zoezi la Oparesheni Kimbunga na kumfikisha kituo cha polisi kwa kuwa alikuwa akiishi nchini kinyume na taratibu za nchi.
“Mauaji ya Shabani Mabadi yamefanyika kama kulipiza kisasi, kwani wakati wa zoezi la Oparesheni Kimbunga marehemu aliwahi kumkamata mtuhumiwa Elias Balandese kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali na kumfikisha katika kituo cha polisi,” alisema Kashai.
Alisema Mbadi alipatwa na mauti wakati akiwa hospitali ya Wilaya ya Kasulu akipatiwa matibabu, kutokana na majeraha aliyokuwa ameyapata.
Wakati huo huo, mtu mmoja amefariki dunia katika Manispaa ya Kigoma Ujiji baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumfunga kamba, miguuni, mikononi na kumfunga kitambaa mdomoni, hali iliyomsababishia kukosa hewa na kufariki dunia
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa