Home » » CHADEMA YAIBANA ACT KIGOMA

CHADEMA YAIBANA ACT KIGOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani hapa, kimetoa siku 14 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhani Maneno kuhakikisha anatoa amri ya kushushwa bendera ya Chama cha ACT katika kijiwe cha CHADEMA, tofauti na hapo sheria zitavunjwa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara juzi, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa, Ally Kisala alisema kuwa Maneno alitoa amri ya kusitisha shughuli zote za kisiasa pamoja na kutopandisha bendera ya chama chochote katika kijiwe hicho baada ya vyama hivyo kukigombania na kuhatarisha amani.
Alisema kuwa kijiwe hicho kilijengwa na CHADEMA lakini baada ya baadhi ya wanachama kuhamia ACT, walitaka pia kijiwe kiwe chao, jambo ambalo lilileta mtafaruku kwa sababu si mali yao.
“Waliohamia ACT walitaka kulazimisha kijiwe kiwe chao na siku iliyofuata walipandisha bendera, kitu kilichotufanya tusikubali na kutoa taarifa kwenye vyombo vya dora ambapo walikuja na kushusha bandera zile,”alisema.
Kisala alisema baada ya mtafaruku huo, mkuu wa wilaya aliwaita viongozi na kufanya nao kikao kisha aliwaandikia barua ya kusitishwa kwa shughuli zozote za kisiasa mpaka hapo ofisi yake itakapojiridhisha.
Kwamba, baada ya agizo hilo, CHADEMA walitii amri hiyo huku ACT wakiendelea kufanya majaribio ya kupandisha bendera yao zaidi ya mara tatu ambapo polisi wamekuwa wakienda kuishusha.
Aliongeza kuwa kama CHADEMA wanaheshimu agizo la serikali lakini wanapuuzwa, hivyo nao wataanza kufikiria kuvunja sheria kama ACT iwapo mkuu huyo hatalipatia muafaka suala hilo ndani ya muda huo.
Chanzo:Tanznia Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa