Home » » CHILONGANI AWA ASKOFU ANGLIKANA

CHILONGANI AWA ASKOFU ANGLIKANA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KANISA la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (Dodoma), limemchagua Mchungaji Dk. Dickson Chilongani kuwa Askofu wa sita wa Dayosisi hiyo katika mkutano Maalum.
Dk .Chilongani amechaguliwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo Godfrey Mhogolo, aliyefariki Aprili mwaka huu akiwa katika matibabu nchini Afrika ya kusini.
Askofu Mteule Dk.Chilongani anashika nafasi hiyo akitokea katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Jimbo wa Kanisa la Anglikana nafasi ambayo amedumu nayo kwa miaka minne.
Dk Chilongani alichaguliwa juzi katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, Dk.Chilongani ambapo alikuwa akishindana na Mchungaji Moses Matonya na Mchungaji Emanuel Madinda ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa Askofu wa nne wa Dayosisi hiyo Yohana Madinda.
Akisoma matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi Askofu wa Tarime Dk. Akili Mwita, alisema kuwa ushindi wa Chilongani ulikuwa wa halali na kwamba baada ya matokeo, wajumbe wa Sinodi maalumu wapatao 748 walikubali na kumuunga mkono.
Novemba 23 mwaka huu atawekwa wakfu katika ibada itakayofanyika katika Kanisa la Roho Mtakatifu na kuongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk. Jakobo Chimeledya.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa