Home » » MASIJALA ARDHI KIGOMA YACHOMWA MOTO

MASIJALA ARDHI KIGOMA YACHOMWA MOTO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WATU wanne wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuchoma moto jengo la masijala ya Idara ya Ardhi Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuteketeza nyaraka mbalimbali.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Japhari Muhamed, alisema jengo hilo liliungua juzi majira ya saa 4 usiku baada ya kuchomwa na watu ambao hawakujulikana.
Alisema kuwa mbinu iliyotumika ni kuchoma ofisi kwa kutumia mafuta ya petroli ambako moto huo uliteketeza ofisi yote na kusababisha hasara kubwa.
“Hakuna kitu kilichosalia baada ya moto kuteketeza ofisi, vyote viliungua zikiwemo hati na nyaraka mbalimbali,” alisema Kamanda Muhamed.
Alisema wanawashikilia watu wanne kuhusiana na tukio hilo ambao ni Anna Fanuel (46), mhudumu wa ofisi, Makrina Paulo (49), karani, Saimon Pius (37), mkazi wa Burega na Tumaini Esau (44), mkazi wa Mwasenga.
Kamanda Muhamed, aliongeza kuwa uchunguzi wa kina dhidi ya tukio hilo unaendelea.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa