Home » » MBARONI KWA TUHUMA ZA KUUA ASKARI

MBARONI KWA TUHUMA ZA KUUA ASKARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

JESHI la Polisi mkoani hapa, linawashikiliwa watu wawili wakazi wa Murubona Wilayani Kasulu kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili akiwemo askari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jaffar Mohamed, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hassani Mussa na Moshi Mussa.
Kamanda Mohamed, alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa na silaha aina ya bastola yenye namba ANC 71T 3818 ikiwa na risasi sita na vocha za mitandao mbalimbali ya simu zinazosadikiwa kuporwa katika duka la Fredrick Joseph, Septemba 30 mwaka huu.
Alisema katika mahojiano ya awali, watuhumiwa hao walikiri kuhusika na mauaji ya Winfrida Evarist mkazi wa Murusi na Askari Polisi yaliyotokea Sikonge mkoani Tabora.
Kamanda Mohamed, alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kufichua wahalifu ili kukomesha vitendo hivyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa