Home » » MUME AUA MKE NA KUTOWEKA

MUME AUA MKE NA KUTOWEKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MWILI wa mwanamke aliyefamika kwa jina la Ekanga Michael (30), umekutwa korongoni maeneo ya Mwanga Vamia karibu na kambi ya jeshi, Manispaa ya Kigoma Ujiji ikidaiwa kuuawa na mumewe.
Akifafanua tukio hilo mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi (ACP), Japhari Muhamed, alisema marehemu aliuawa baada ya kupigwa  sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema kuwa, uchunguzi ulibaini kwamba aliyehusika na kifo hicho ni mume wake aitwaye Cyprian Kagaruki, baada ya kutokea ugomvi baina yao uliosababisha mumewe  kufikishwa mahakamani na hatimaye kupelekwa gerezani.
“Baada ya mumewe kupata dhamana, alirudi nyumbani na kulipiza kisasi kwa mke wake kwa kumpiga hadi kumuua na hatimaye akakimbia,” alisema Kamanda Muhamed.
Aliongeza kuwa, kabla ya mauaji wana ndoa hao walitoka nyumbani asubuhi na baadaye alirudi mume pekee na Septemba 15 majira ya saa 3:30 asubuhi, mke alionekana korongoni akiwa amekufa.
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na msako ili kumkamata mtuhumiwa na hatimaye kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa