Home » » TAMWA KIMELANI VITNDO VYA WANAUME KUTELEKEZA FAMILIA ZAO.

TAMWA KIMELANI VITNDO VYA WANAUME KUTELEKEZA FAMILIA ZAO.

 
Kufuatia ongezeko la baadhi ya wanaume wanaozitelekeza familia zao kwa kisingizio cha maisha magumu chama cha waandishi wa habari wanawake nchini- TAMWA kimelaani vitendo hivyo na kubaini njia pekee ya kutatua tatizo hilo ni vyombo husika kuwachukulia sheria kali ili iwe fundisho ambpo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake wanaojitokeza mara baada ya kutelekezwa na kuishi maisha ya kutegemea kusaidiwa kwa kuomba msaada kwa watu binafsi na katika vyombo vya habari.
ITV imezungumza na Bi Judidhi Jumanne mkazi wa Singida aliyetelekezwa na mume wake akiwa na ujauzito waa mienzi minne baada ya kuishi nae kwa muda mrefu ambapo kwa uchungu amesema mara baada ya kutelekezwa alilazimika kulea ujauzito huo peke yake bila kujua mwanaume alikotokomea nana kubaini maisha anayoishi ya kusaidiwa na majirani mara baada ya kuijifungua kwa oparesheni huku mtoto akiwa na tatizo la kukosa tundu la kujisaidia haja kubwa na hivyo kutobolewa ubavuni.
 
Baadhi ya majirani waliobeba jukumu la kumsaidia binti huyo wameendelea kulaani vikali vitendo hivyo na kuviita vya kinyama huku wakiiomba vyomba husika kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho.
 
Mkurugenzi mtendaji chama cha waandishi wa habari wanawake nchini TAMWA Bi Valeria Msoka amekiri ongezeko kubwa la matatizo ya wanawake kuendelea kutelekezwa kutokana na wengi kutokujua haki zao za msingi na kutoa wito kwa mashirika,taasisi na vyombo vya dola kushirikiana ili kuwachukulia sheria kali wale wote wanaobainika kufanya hivyo.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa