Home » » KAFULILA: TANZANIA IWAJIBIKE KUREJESHA AMANI YA BURUNDI.

KAFULILA: TANZANIA IWAJIBIKE KUREJESHA AMANI YA BURUNDI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
mbunge wa kigoma kusini (nccr-mageuzi), david kafulila.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, (pichani) amesema Tanzania inapaswa kuwajibika kuhakikisha amani inarejea Burundi na nchi nyingine za maziwa makuu ili nayo iendelee kuwa imara.
 
Akichangia katika mkutano wa pili wa Umoja wa Wabunge Vijana Duniani chini ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), uliofanyika jijini Tokyo, Japan juzi, Kafulila alisema Tanzania inapaswa kuhakikisha amani kwa nchi majirani kwa kuwa amani hiyo ni muhimu kwa Tanzania.
 
“Tanzania inatumia muda na rasilimali nyingi kuhakikisha usalama wa nchi za maziwa makuu siyo kwa sababu haina imani au inapenda kufanya kazi hizo bali kwa sababu usalama wa raia wa nchi za maziwa makuu ni muhimu sana kwa uimara wa Tanzania kihistoria, kijamii na hata kiuchumi kwani watu hawa tunaingiliana sana kihistoria na hivyo utu wao ni muhimu sana kwetu kama ndugu zetu,” alisema Kafulila katika taarifa yake aliyoituma kwa NIPASHE jana.

CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa