Home » » TAASISI YA MISS TANZANIA 2012, BRIGITTE ALFRED YATOA MAFUNZO KWA ALBINO 20 KIGOMA

TAASISI YA MISS TANZANIA 2012, BRIGITTE ALFRED YATOA MAFUNZO KWA ALBINO 20 KIGOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

unnamed (69)
.Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akizindua ujenzi wa bweni la Albino Buhangija mkoani Shinyanga.
unnamed (70)
Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi yake ya BAF ambayo kwa kushirikiana na Junior Achievement (JA) huku lengo kuu likiwa ni kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa albino Tanzania nzima. Kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), Mohamed Chanzi.
unnamed (71)
Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Albino mara baada ya kuzindua mafunzo ya Ujasiriamali Makumbusho ya Taifa.
……………

Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) kwa kushirikiana na Taasisi ya Junior Achievement (JA)  imeendeleza zoezi la kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wajamii ya watu wenye albino nchini.Mafunzo hayo ya wiki mbili yalifunguliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma ambapo jumla ya albino 20 walifaidika na mafunzo hayo yaliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma, kanali mstaafu Issa Machibya. Mbali ya watu wenye albino, washiriki wengine katika mafunzo hayo walikuwa wanawake na vijana.
 
Machibya alitoa wito kwa taaisis nyingine kuiga mfano taasisi ya Brigitte na Junior Achievements ambayo mpaka sasa imetoa mafunzo kama hayo kwa vijana na akina mama 25,000.Mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa mafunzo ya ujasiliamari ni muhimu kwa kila mtu na kupongeza juhudi za mrembo huyo ambaye mpaka sasa ametoa mafunzo kwa watu wenye albino 70. Kati ya hao 70, albino 50 walipata mafunzo jijini Dar es Salaam.
 
 “Haya ndiyo mambo muhimu ya kuigwa kwa jamii, taasisi ya Brigite imetoa elimu ambayo itawawezesha wahitimu kufanyakazi ya ujasiriamali na kujipatia kipato kwa jasho lako, nawapongeza sana na taasisi nyingine zifuate nyayo,” alisema Mashibya.Mratibu wa mafunzo hayo, Stanley Mosha alisema kuwa kwa kupitia BAF kwa sasa unaende vizuri na lengo lao ni kutoa mafunzo kwa watu wenye albino kila mkoa na wamepanga kutoa mafunzo kwa albino 300 nchi nzima kwa mwaka 2015.
 
Mosha alisema kuwa lengo lao mafunzo hayo ni kuwawezesha kiuchumi vikundimbalimbali hususani vijana na wakinamama. Alisema kuwa hatua hiyo imetokana na mafanikio ya Brigitte katika mashindano ya urembo ya Dunia ya mwaka 2013  nchini Indonesia na kushika nafasi ya tatu kupitia taji la mrembo mwenye malengo baada ya kuonyesha dunia jitihada zake za kusaidia watu wenye ualbino nchini Tanzania.
 
Alisema kuwa kuanzia hapo, Brigitte amekuwa Balozi wa watu kwa watu wenye ualbino Tanzania na kufanya shughuli mbalimbali za kuwasaidia mfano ujenzi wa bweni la kisasa lenye uwezo wa kuchukua idadi ya watoto 60, na uboreshaji  mazingira kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga.
 
“Nimefuraishwa na Mwitikio na ushirikiano walioonyesha kwa kutambua na kukubali kuliingiza kundi hili na kuweza kuungana na makundi mengine ya vijana katika program za ujasiriamali. Kulitambua na kulijumuisha kundi hili katika kuwajengea uwezo ni hatua kubwa inayowezesha kupanua wigo na juhudi za kuwezesha makundi ya vijana na wakinamama kiuchumi na tunaomba wadau wengine waungane nasi katika hili,” alisema Mosha.
 
Kwa upande wake, Brigitte alisema kuwa ataendeleza mpango huo hapa nchini na anaamini atafikia lengo lake. “Nashukuru Junior Achievement kwa kuniunga mkono katika mpango huu ambao kwa sasa unapata mafanikio makubwa, naomba kuungwa mkono kwani jukumu hili ni la watanzania wote,” alisema Brigitte.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa