Home » » CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KIGOMA CHAWATUMBUA WALIOSALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KIGOMA CHAWATUMBUA WALIOSALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala akiongea na waandishi(ambao hawapo pichani) juu ya wanachama 25 waliowafuta uanachama kwasababu ya kukisaliti cha wakati wa uchaguzi mkuu oktoba mwaka jana.
Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala akielekezana jambo kwenye ilani ya chama na katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa Stanely Mkandawile kulia ni Daniel Gorge Katibu msaidizi kigoma vijijini

Na Editha Karlo,wa blog ya jamii, Kigoma.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Kigoma kimewafukuza uanachama 25 wa chama hicho baada ya kukisaliti chama kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Okt0ba 25 Mwaka jana.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa CCM Mkoa  Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala alisema kuwa uamuzi huo wa kuwafuata uanachama ulitolewa na kikao cha halmashauri kuu cha Mkoa kilichofanyika tarehe 2 march mwaka huu.

Naomi alisema kuwa baaada ya uchaguzi mkuu kufanyika chama kilianza kufanyatathimini na changamoto walizokutana nazo kipinchi cha uchaguzi mkuu.

''Kwenye tathimini yetu hiyo tuliweza kugundua kuna baadhi ya wanachama ambao walikuwa siyo waaminifu kipindi cha uchaguzi mkuu walikuwa wakikisaliti chama tena wengine walikuwa viongozi na wengine waliogombea ubunge na kushindwa kwenye  kura za maoni tumeamua watupishe sisi tuendelee kutekeleza ilani ya chama''alisema Kapambala.

Aliwataja wanachama waliofukuzwa uanachama kuwa ni pamoja Venance Mpologomi,Paul bahinda, Damasi Shetei,Gidioni Bunyanga,Edger Mkosamali,Pili Waziri,Pendo Jumanne,Robinson Lembo na Juma matete.

Wengine waliofukuzwa uanachama ni Idd Lugundanya,Juma Kifuku,Edga Bisoma,Staphord Kumuhanda,Jenoveva Bisana,Salehe Anatori,Abdallah Chugu,Atanas Andrea,Bigilimana Vyanda,Jonas Kafyiri,Isack Braytony,Christopher Chiza,Fanuel Kasogota,Laulent Bikulamuchi,Ibramu Shikuzilya na Paul Chabandi.

Alisema wanachama hao walifukuzwa uanachama wa chama cha mapinduzi tayari wameshahamia vyama vingine pia tathimini ya uchaguzi Mkuu  bado inaendelea.

Naye Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Kigoma Staney Mkandawile alisema kuwa sasa hivi kazi iliyopo ni kutekeleza ilani ya chama na kuumunga mkono  Rais John Magufuli kauli mbiu ya hapa kazi tu.

''Chama hakitamuonea mtu yeyote,ni bora tubaki wachache ndani ya chama lakini tuwe tunatekeleza ilani ya chama na kukipenda chama"Alisema Mkandawile

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa