Home » » SHIRIKISHO LA MPIRA UEFA YAKABIDHI MIPIRA 60 KIGOMA

SHIRIKISHO LA MPIRA UEFA YAKABIDHI MIPIRA 60 KIGOMA


NA MAGRETH MAGOSSO,KIBONDO.

SHIRIKISHO la Mpira Barani Ulaya (UEFA) kwa kushirikiana na Kampuni ya kutengeneza magari ya Chivrolet ya Marekani imewakabidhi  mipira 60 kwa  ajili ya Soka la  Watoto walio chini ya miaka 12 kwa shirika la Umoja wa Mataifa UNHCR la kuhudumia wakimbizi katika Kambi ya Nduta iliyopo wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenye kambi ya Mtendeli zote za Mkoa wa Kigoma .

Akithibitisha hilo juzi Mkuu wa UNHCR Kibondo Dost Yousafzai alisema wamepokea mipira hiyo kwa nia ya kuwaunganisha  na kuthaminiana baina ya watanzania na warundi katika tasnia ya michezo hususani katika soka la mpira wa miguu kwa watoto waishio kambini kwa kuwa wafrika wote ni ndugu .

Alisema pamoja na UEFA na kampuni hiyo kutoa kwa ajili ya kambi hizo,shirika la UNHCR wametoa mipira 20 kwa ajili ya vijiji vinavyoishi karibu na kambi ya nduta ya kibondo na mipira 20 kwa vijiji vinavyoishi jirani na kambi ya mtendeli,ili waratibu wa chama cha mpira wilayani humo wagawe kwa timu hai ili kuimarisha michezo baina ya raia na wakimbizi.
  
Akipokea mipira hiyo kwa niaba ya wanakijiji  Katibu wa Chama cha mpira Kibondo James Evalist alisema kwa leo anachukua mipira 10 tu,na mipira miwili aliikabidhi kwa timu ya Birutana ambayo inashiriki mashindano ya mechi za ujirani mwema baina ya Burundi na Tanzania huku mipira 10 ikisalia kwa mkuu wa UNHRC.


’ mipira ya watoto haihimili vishindo kwa timu za wakubwa, siikatai na nawashirikisha wanamichezo wa kibondo lakini  kama mmeamua kutusidia mlete mipira inayokidhi mahitaji ya timu za wakubwa lakini tunaomba mturekebishie uwanja wa Mpira kwa kuwa uwanja uliopo ni una kokoto tupu, alisema James. 

Naye Kaimu Mkuu wa makazi Kambi ya Nduta Jesca Ntaita alitoa mwito kwa  Watanzania na Warundi wanaoishi katika makambi ya wakimbi kufuata taratibu za nchi kwa kuwa kuna baadhi ya watanzania huingia makambini kwa vibali vya warundi na warundi vivyo hivyo.

Na Mtendaji wa kijiji cha Biturana Henry Thomas alisihi shirika la UNHCR  kuwa waendeleze mashindano ya ujirani mwema baina ya raia wa pande zote mbili waishio katika kambi hizo,kuwa yasiishie kambini bali yaongeze wigo wa mashindano hayo.
                                                         
Aidha kudhihirisha kuwa wanaweza kusakata kabumbu timu ya kambi ya mtendeli iliwabugiza goli 4-0 dhidi ya   Timu ya kijiji cha Kasanda  huku timu ya kambi ya nduta iliwafunga bao 2 Timu ya Kijiji cha Biturana ya wilayani.mwisho.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa