Home » » WAZAZI WAPONGEZWA MUAMKO WA ELIMU

WAZAZI WAPONGEZWA MUAMKO WA ELIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WAZAZI mkoani hapa wamepongezwa kwa kuwa na muamko wa kuwasomesha watoto wao katika shule zinazokidhi mahitaji ya wanafunzi bila kujali hali duni za familia zao.
Akizungumza katika mahafali ya kuhitimu Kidato cha nne Shule ya Sekondari Mugaba iliyoko kijiji cha Nyakitonto, Wilaya ya Kasulu mkoani hapa, Ofisa Elimu Shule za Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya hiyo,  Patrick Athanas, alisema kuwa wazazi wengi huogopa kuwapeleka watoto wao shule za binafsi kwa kuhofia kushindwa kulipa ada.
Alisema kuwa ni jambo la msingi kwa wazazi kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto katika maisha yao ya baadae bila kujali kupoteza pesa nyingi, kwani mtoto akipata elimu atakuwa na uwezo wa kujitegemea sambamba na kuwasaidia wazazi.
Athanas, alisema kuwa wakati shule ya Sekondari Magaba inaanza, ilianza na wanafunzi wengi na hata sasa ina wanafunzi wengi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kutoka ndani ya Mkoa wa Kigoma na hata mikoa mingine ya Tanzania, hii inaonyesha kuwa wazazi wa Mkoa huu hawaangalii pesa bali wanaangalia elimu kwa watoto wao.
“Nampongeza sana mmiliki wa shule hii Leonard Magaba kupata maono haya ya kujenga shule ambayo inakidhi mahtaji ya wanafunzi hasa kwa kuwa na maabara, maktaba, vitabu, umeme, maji na walimu wa kutosha” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa