Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chote ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma akisisitiza jambo kwa washiriki hao wakati akifunga mafunzo hayo.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akizungumza muda mfupi kabla ya Hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika Mjini Kigoma. (Picha na Frank mvungi-Maelezo)
Frank Mvungi - Maelezo.
Serikali
imewataka watumishi wa umma katika mikoa na Halmashuri kubadilika na
kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mabadililko ya mifumo
yanayofanywa kwa kushirikina na wadau wa maendeleo.
Akizungumza
wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa kielektroniki utakaotumika kuandaa
mipango,bajeti na kutoa ripoti yaliyowashirikisha washiriki kutoka Mikoa
ya Katavi, Rukwa na kigoma, Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Dkt. Paul Chote amesema dhamira ya
serika ni kuwawezesha watumishi wake kutekelza majukumu yao kwa ufanisi
hasa katika kuwahudumia wananchi.
“Mfumo
huu sio wa majaribio hivyo ni wajibu wa kila mshiriki kurudi katika
mkoa na halmashuri na kuhakikisha kuwa anajenga uwezo kwa watumishi
ambao hawakushiriki katika mafunzo haya kwa kuwa mfumo huu unahitaji
uwajibikaji wa pamoja” alisisitiza Chote.
Akifafanua
Dkt. Chote amesema kuwa washiriki wa mafunzo hayo wana jukumu kubwa
lakutumia weledi na ujuzi waliopata kuleta mageuzi chanya katika maeneo
yao ili azma ya serikali kutoa huduma bora itime.
Kwa
upande wake Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Lisa Rwamiago
amesema kuwa vituo zaidi ya elfu 22,000 vya kutolea huduma
vitaunganishwa katika mfumo huo wa Kitaifa hali itakayofanya Tanzania
kuwa nchi ya kwanza kusini mwa Afrika kwa kuwa na mifumo bora yakutolea
huduma.
0 comments:
Post a Comment