Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias
Kwandikwa (Mb), akizungumza na uongozi wa wilaya ya Kakonko, alipokuwa
katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya
Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias
Kwandikwa (Mb), akikagua kalvati katika barabara ya Nyakanazi-Kibondo
KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias
Kwandikwa (aliyevaa suti) akikagua matofali katika kambi ya mkandarasi
ya Nyanza Road Works alipokuwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa
ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango
cha lami. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa
Kigoma Eng. Narcis Choma.
Meneja
wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura, akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), ya mradi wa ujenzi wa barabara ya
Nyakanazi-Kibondo KM 50 inaojengwa kwa kiwango cha lami. Kulia ni Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.
Meneja
wa mradi kutoka Kampuni ya Nyanza Road Works Massimo Cartura (kulia),
akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), aina ya kokoto zinazotumika katika
ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 inayojengwa kwa kiwango
cha lami. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa
Kigoma Eng. Narcis Choma.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias
Kwandikwa (Mb), akisisitiza jambo kwa Meneja wa mradi kutoka Kampuni ya
Nyanza Road Works Massimo Cartura (kushoto), wakati akikagua ujenzi wa
barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50 kwa kiwango cha lami, mkoani Kigoma.
Mhandisi
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo KM 50
inayojengwa kwa kiwango cha lami Dunaka Screenivasa Rao akifafanua jambo
kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Mhe. Elias Kwandikwa (Mb), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi huo
mkoani Kigoma.
………………
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa
Elias Kwandikwa (Mb), ametoa muda wa siku 21 kwa Mkandarasi Nyanza Road
Works kuongeza vifaa vya kazi na wafanyakazi ili kuongeza kasi ya ujenzi
wa barabara ya Nyakanazi-Kibondo yenye urefu wa KM 50 inayojengwa kwa
kiwango cha lami.
Mhe.
Kwandikwa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma leo, wakati akikagua maendeleo
ya ujenzi wa mradi huo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa
ujenzi huo unatakiwa kukamilika haraka ili kuweza kufungua mkoa huo na
kurahisha shughuli za usafirishaji.
“Hakikisheni
ndani ya wiki tatu vifaa vya ujenzi vinakuwepo eneo la kazi na ajira
zinatolewa kwa wananchi ili mradi ukamilike mapema iwezekanavyo”,
amesisitiza Mhe. Kwandikwa.Kuhusu
suala la malipo, Mhe. Kwandikwa amefafanua kuwa hivi sasa hakuna tatizo
lolote la malipo kwani mkandarasi ameshalipwa na kilichobaki sasa ni
mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili ujenzi ukamilike.
“Tunamshukuru
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi anazozifanya kwani hivi
sasa hali ya fedha ni nzuri, mapato yanaongezeka hivyo tutegemee kupata
matunda ya maendeleo ya miundombinu bora hapa nchini”, amesema Naibu
Waziri Mhe. Kwandikwa.
Aidha,
Naibu Waziri amewataka makandarasi wazawa kuongeze juhudi kubwa katika
miradi ya ujenzi hapa nchini hadi kufikia zaidi ya asilimia 60 ili
waweze kupewa fursa za miradi mingi ya ujenzi wa barabara.“Kazi
za wazawa zikifanya vizuri na vijana wetu wakifanya kazi kwa uadilifu
na uzalendo kutaongeza tija katika maendeleo ya miundombinu nchini na
hatua nzuri ya kufikia katika uchumi wa kati”, amesema Mhe. Kwandikwa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagalla, amesema kwa
niaba ya wananchi wake wanaungojea mradi huo ukamilike kwa wakati na
ubora ili kuondoa adha wanazozipata hasa vipindi vya mvua.
Naye
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis
Choma, amemuahidi Mhe. Kwandikwa, kuwa atamsimamia mkandarasi na
kuhakikisha kasi ya ujenzi inaenda sambamba na vifaa pamoja na
wafanyakazi.
Mkakati
wa Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya
barabara katika ukanda wa magharibi ili kuiwezesha kufanya biashara
kiurahisi na mikoa mingine ya Tanzania na nchi za Congo DRC, Rwanda na
Burundi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 comments:
Post a Comment