Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kiongozi
wa Timu ya wataalamu wanaofanya maboresho ya mfumo wa kielektroniki wa
PlanRep, Bi. Nseya Kipilyango akizungumza wakati wa mafunzo kwa
watumiaji wa mfumo huo yanayoendelea Mjini Kigoma.
Mmoja
wa Wawezeshaji wa Mfumo wa mfumo wa kielektroniki wa PlanRep Kutoka
Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Jacqueline Manyanga akiwasilisha mada kwa
watumiaji wa mfumo huo yanayofanyika Mkoani Kigoma yakihusisha Mikoa ya
Rukwa, Katavi na Kigoma.
Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Kigoma.
Tanzania
imetajwa kuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Afrika kuanza kutumia mfumo wa
kielektroniki wa PlanRep ulioboreshwa ambao husaidia katika mipango,
bajeti na kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini
kote.
Akizungumza
katika mahojiano maalum mjini Kigoma, Mkuu wa Timu ya Mifumo ya TEHAMA
kutoka mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Desderi
Wengaa, amesema kuwa mfumo huo utasaidia Taifa kufikia maendeleo
endelevu kwa wakati kwani utaunganishwa na mifumo mingine iliyopo sasa
na utawashirikisha wananchi wote.
“Mfumo
huu utawezesha kutolewa kwa taarifa za miradi ya maendeleo zinazohusu
sekta zote zilizoainishwa katika mipango na bajeti kwa wakati katika
kipindi chote cha mwaka” alisema Wengaa.
Aliendelea
kusema kuwa PlanRep iliyoboreshwa inaunganisha sekta zote katika mfumo
mmoja ambao ni wa kitaifa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kila sekta
ilikuwa na mfumo wake. Awali mfumo uliokuwa ukitumika haukuwa unaendana
na mahitaji ya wakati hivyo kushindwa kufanya uchambuzi wa kina katika
kusimamia rasilimali zilizokuwepo ikiwemo fedha.
Aidha,watumiaji
wa mfumo huo wataweza kuutumia mahali popote kwa kuwa ni wa kitaifa
na utaondoa changamoto ya kuwepo kwa matoleo tofauti tofauti. Hali hii
itasaidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika kwa watoa huduma wa
mifumo ya awali katika halmashauri na mikoa yote nchini.
Kuwepo
kwa mradi wa maboresho ya mifumo katika sekta za umma (PS3) kumesaidia
wataalamu wa TEHAMA na watumiaji wengine wa mfumo wa PlanRep
iliyoboreshwa kujengewa uwezo ili kuimarisha utendaji wao katika
kuwahudumia wananchi. Miongoni mwa wanufaika wa mfumo huu ni waganga
wakuu,wachumi, maafisa mipango, makatibu wa afya na watoa huduma katika
ngazi mbalimbali hasa katika zahanati, vituo vya afya na shule.
Kuunganishwa
kwa mfumo huu katika mifumo ya malipo, kukusanya mapato, kukusanya
taarifa za sekta ya afya na mifumo mingine iliyokuwepo awali kutawezesha
uchambuzi wa bajeti kufanyika kwa njia ya mtandao, hivyo kuifanya
Mikoa, Wizara, halmashuri na taasisi za Serikali kuwa na toleo moja la
bajeti.
Mfumo
wa PlanRep iliyoboreshwa umetengenezwa na wataalamu wazalendo hivyo
itakuwa rahisi katika kufanya maboresho endapo yatahitajika kwa
kuzingatia mahitaji ya wakati na mikoa husika. Mradi huu wa kuboresha
mifumo ya sekta za umma unatekelezwa katika Mikoa 13, Halmashauri 93 na
baadaye utatumika nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment