Home » » WAKAZI WILAYA YA KAKONKO WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF-KIGOMA‏

WAKAZI WILAYA YA KAKONKO WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF-KIGOMA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Katibu tawala wilaya ya Kakonko Bi.Zainab Mbunda akifungua Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Afya ya Jamii CHF uliofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko huo wa hiari ambao unawawezesha kupata huduma za matibabu kwa muda wa mwaka mzima baada ya kujiunga na kuchangia kiasi cha shilingi elfu kumi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko Bi.Jaina Msangi akizungumza namna ambavyo Halmashauri inavyosimamia Mfuko huo wa CHF na kueleza kuwa wamekuwa wakihamasisha Jamii kujiunga na Mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma za Afya.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw.Rehan Athuman akitoa maelezo mafupi kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii CHF na namna ambavyo ulivyoweza kuwafikia watanzania na kunufaika na huduma za Mfuko huo unaolenga kuboresha afya za wananchi hususani wenye kipato cha chini na cha kati.
Baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya waliohudhuria katika Mkutano huo wakiwemo Madiwani,Watendaji wa vijiji,Kata na Vitongoji,Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa,Mashirika,Asasi mbalimbali na Wazee Maarufu wa wilaya ya Kakonko(Picha zote na  KAPIPIJhabari.COM) 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa