Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Soko
la Kijiji cha Ndago,wilayani Iramba lililoshindikana kukamilishwa kwa
meza za kufanyia biashara kwa wananchi wa Kijiji hicho kutokana na TASAF
awamu ya pili kujitoa kukamilisha ujenzi wa meza hizo kwa kukosa fedha
za kufanyikazi hiyo,baada ya kutotengwa kwa fedha za kazi hiyo.(Picha
zote na Jumbe Ismailly).
Na Jumbe Ismailly, Iramba
MFUKO
wa Maendeleo ya jamii (TASAF) Wilaya ya Iramba,Mkoani Singida
umeshindwa kukamilisha ujenzi wa meza za soko la Kijiji cha Ndago kwa
zaidi ya miaka mitano sasa baada ya awamu ya tatu ya mpango huo
kumalizika kutokana na kutokuwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya kazi
hiyo.
Kutokana
na meza kutokamilika kumechangia soko hilo kutoanza kutumika na hivyo
kuwafanya baadhi ya wafanyabiashara wa Kijiji hicho kufanya ufunguzi
usio rasmi na kuanza kupanga biashara ndogo ndogo kama vile
nyanya,vitunguu na viazi vitamu chini kwenye sakafu.
Baadhi
ya madereva wa bodaboda wa Kijiji cha Nguvumali,kata ya Ndago
walibainisha hayo kwa nyakati tofauti walipokuwa wakiongea na gazeti
hili lililotaka kufahamu sababu za kutokamilika kwa soko hilo kwa muda
merefu sasa ili liweze kuanza kutumiwa na wananchi wa maeneo hayo.
Madereva
hao wa bodaboda,Abeli Julius Nkengele,mkazi wa Kijiji cha Nguvumali
alifafanua kuwa kuendelea kuchelewa kukamilika kwa soko hilo kunazidi
kuongeza gharama za ujenzi wa meza kupanda huku soko likizidi kuendelea
kuchakaa na hivyo kuifanya serikali kuingia gharama zingine kubwa kuliko
zile zilizokadiriwa kutumika.
Bodaboda
hao walifafanua kuwa kukosekana kwa huduma katika soko kunawakosesha
mapato katika biashara wanayofanya na kuongeza kuwa kuwepo kwa soko hilo
kutawasaidia kupata wateja wenye mizigo inayohitajika kubebwa kwa
kutumia usafiri wa pikipiki zao.
“Kuhusu
habari ya soko yaani mpaka sasa hivi lilivyofikia,vitu vinazidi kupanda
bei na soko linazidi kuchakaa,kwa hiyo serikali itazidi kuingia gharama
nyingine ndefu kulikoni kwa sababu vitu madukani vinapanda bei na soko
linazidi kuchakaa”alisisitiza Nkengele.
Kwa
mujibu wa Nkengele aliishauri serikali kufanya utaratibu wa kuhakikisha
soko hilo linakamilika na kuanza kutumiwa na wananchi wa Kijiji hicho
kama ilivyokusudiwa na mpango wa Tasaf awamu ya tatu,jambo
litakalowasaidia hata wao kupandisha mapato yao kwa siku.
Kwa
upande wake mkazi wa Kijiji cha Nguvumali,Peter Maiko ambaye pia ni
dereva wa bodaboda aliweka wazi kwamba kutokamilika kwa soko hilo
kunatokana na uongozi mbovu wa Kijiji cha Ndago kwa kushindwa kufuatilia
wilayani na kusimamia kikamilifu ili meza hizo ziweze kujengwa.
“Kama
ni uongozi umeshashindwa basi wakabidhi wafanyabiashara ili wafanye kwa
mkataba,ili mtu ajenge meza na akishamaliza afanye biashara mpaka
gharama zake zitakapofikia ndipo aendelee kulipa ushuru wa soko,maana
tunahitaji kufanyakazi hapa sokoni”alifafanua Maiko.
Akizungumzia
malalamiko ya wananchi wa Kijiji hicho,diwani wa kata ya Ndago,Shabani
Lyanga Msholo alisema soko hilo lililokuwa likijengwa na tasaf awamu ya
pili haliweze kuendelea kujengwa tena kutokana na fedha zilizotengwa kwa
kazi hiyo kumalizika na hivyo kwa sasa wananchi wanatakiwa kuchanga
fedha za kumalizia ujenzi wa meza katika soko hilo.
Franki
Kitundu ni afisa mtendaji wa kata ya Ndago licha ya kukiri kukosekana
kwa meza katika soko hilo,lakini hata hivyo alisema kuchelewa kuanza
kutumika kwa soko hilo kunatokana na kukosekana fedha za kumalizia
ujenzi huo na kuongeza kuwa hakuna fedha zozote zilizotolewa kwa
serikali ya Kijiji,bali Tasaf ndiyo wanafahamu zilipo fedha za kumalizia
ujenzi wa meza hizo.
Halima
Mpita ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba alisema
tasaf awamu ya pili ilishajitoa kukamilisha soko hilo kwa hivyo
Halmashauri inaendelea kutafuta fedha kwenye vyanzo vyake ili iweze
kukamilisha ujenzi wa meza hizo haraka iwezekanavyo.
0 comments:
Post a Comment