Home » » Watumishi 9 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wasimamishwa kazi

Watumishi 9 wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wasimamishwa kazi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu akizungumza na waandishi wa habari hii leo kuhusu kusimamishwa kazi kwa watumishi 9 wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji. (Picha na Emmanuel Senny) (2)
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndungulu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusimamishwa kazi kwa watumishi 9 wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji. (Picha na Emmanuel Senny).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu mwenye suti nyeusi, akizungumza na waandishi wa habari hii leo kuhusu kusimamishwa kazi kwa watumishi waManispaa ya Kigoma-Ujiji. (Picha na Emmanuel Senny) (2)
Na Emmanuel Senny, Kigoma
Watumishi tisa wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji wamesimamishwa kazi mara baada ya kubainika kuingia mikataba mibovu isiyokuwa na tija na kuisababishia manispaa hasara ya kupoteza mapato sambamba na kulipa fidia ambazo ni batili pamoja na kuuza mali za halmashauri kinyume cha sheria.
Maamuzi hayo yamefikiwa na ofisi ya Mkoa wa Kigoma baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, kubaini uuzwaji huo na kumuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huu, kufanya uchunguzi wa awali kuhusu  tuhuma hizo ambapo alitakiwa kutoa mrejesho Januari 2 katika ofisi ya Waziri Mkuu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndungulu, amesema, baada ya kuagizwa na Waziri Mkuu, aliunda kamati ya uchunguzi wa awali ambapo kabla ya Januari 2 walikuwa wameshakamilisha uchunguzi wa tuhuma hizo.
Alisema kuwa, awali tuhuma ambazo alizibaini Waziri Mkuu ni pamoja na uuzwaji wa majengo ya Manispaa likiwemo Jengo la Maendeleo ya Mkoa (KIGODEKO) lenye kiwanja namba 551 na Miboss lenye kiwanja namba 295 ambapo watuhumiwa walidai kuwa waliuza viwanja badala ya majengo.
“Tuhuma zingine zinazowakabiri watumishi hao ni manunuzi hewa ya vipuri vya gari SM 553 gari aina ya tipa vyenye gharama ya TSH. 8,002,000, Ununuzi hewa wa sajala yenye thamani ya Tshs. 4,640,000, matumizi mabovu ya fedha za serikali kwa ajiri ya matengenezo ya barabara yenye thamani ya Tsh. 18,000,000 kwa ajiri ya matengenezo na Tsh. 48,000,000 kwaajiri ya mkataba ambao haukufanyiwa kazi na matumizi yasiyoidhinishwa ya Tshs. 809,633,407 ambazo zilitengwa kwaajiri ya miradi ya maendeleo badala yake zikapelekwa kwenye ujenzi wa maabara,” amesema Ndungulu.
Aidha Ndungulu amesema, uchunguzi wa awali uliofanywa na  kamati ulibaini kuwa watendaji wa manispaa waliingia mikataba mibovu isiyokuwa na tija na kuisababishia manispaa hasara ya kupoteza mapato sambamba na kulipa fidia ambazo ni batili, baadhi ya watendaji kushiriki katika ubadhilifu wa uuzwaji wa mali za manispaa bila kufuata utaratibu, ukodishaji wa jengo la KIGODEKO bila kufuata sheria.
Ndungulu amesema, baada ya kubainika kwa tuhuma hizo ofisi ya mkoa imeamua kuwasimamisha kazi watumishi hao ili kupisha uchunguzi zaidi kuhusu tuhuma hizo ambapo uchunguzi zaidi ukikamilika hatua zingine za kisheria zitafanyika.
Aliwataja majina watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Wilfred Mwita (Mkuu wa Idara ya  Mipango  Manispaa), Emmanuel Mkwe (Mwanaseheria wa Manispaa), Mhandisi Boniface William (Mhandisi wa Manispaa), Mussa Igugu (Mkuu wa Kitengo cha Biashara), Elimboto Zacharia (Mkaguzi wa Ndani wa Manispaa), Leonard Nzirailunde (Afisa Misitu), Shida Thadei (Afisa Ugavi), Gwawili Mkoka (Mhasibu wa Manispaa) na Omary Hassan (Fundi Mkuu wa Magari).
Hata hivyo Ndungulu alisema, Ofisi ya Mkoa imemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri Mhandisi, Boniface Nyambele, kusimamia urejeshwaji wa mali za Manispaa zilizouzwa bila kufuata sheria na taratibu.
“Pia tumewaagiza jeshi la polisi na TAKUKURU kuchunguza tuhuma hizo kama kuna mianya ya rushwa ili kama kuwa watu walihusika katika utoaji wa rushwa basi nao washughulikiwe kwa mujibu wa sheria,” alisema Ndunguru.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa