Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndungulu akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu kusimamishwa kazi kwa watumishi 9 wa Manispaa ya
Kigoma-Ujiji. (Picha na Emmanuel Senny).
Na Emmanuel Senny, Kigoma
Watumishi
tisa wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji wamesimamishwa kazi mara baada ya
kubainika kuingia mikataba mibovu isiyokuwa na tija na kuisababishia
manispaa hasara ya kupoteza mapato sambamba na kulipa fidia ambazo ni
batili pamoja na kuuza mali za halmashauri kinyume cha sheria.
Maamuzi
hayo yamefikiwa na ofisi ya Mkoa wa Kigoma baada ya Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, kubaini uuzwaji
huo na kumuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huu, kufanya uchunguzi wa awali
kuhusu tuhuma hizo ambapo alitakiwa kutoa mrejesho Januari 2 katika
ofisi ya Waziri Mkuu.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndungulu,
amesema, baada ya kuagizwa na Waziri Mkuu, aliunda kamati ya uchunguzi
wa awali ambapo kabla ya Januari 2 walikuwa wameshakamilisha uchunguzi
wa tuhuma hizo.
Alisema
kuwa, awali tuhuma ambazo alizibaini Waziri Mkuu ni pamoja na uuzwaji
wa majengo ya Manispaa likiwemo Jengo la Maendeleo ya Mkoa (KIGODEKO)
lenye kiwanja namba 551 na Miboss lenye kiwanja namba 295 ambapo
watuhumiwa walidai kuwa waliuza viwanja badala ya majengo.
“Tuhuma
zingine zinazowakabiri watumishi hao ni manunuzi hewa ya vipuri vya
gari SM 553 gari aina ya tipa vyenye gharama ya TSH. 8,002,000, Ununuzi
hewa wa sajala yenye thamani ya Tshs. 4,640,000, matumizi mabovu ya
fedha za serikali kwa ajiri ya matengenezo ya barabara yenye thamani ya
Tsh. 18,000,000 kwa ajiri ya matengenezo na Tsh. 48,000,000 kwaajiri ya
mkataba ambao haukufanyiwa kazi na matumizi yasiyoidhinishwa ya Tshs.
809,633,407 ambazo zilitengwa kwaajiri ya miradi ya maendeleo badala
yake zikapelekwa kwenye ujenzi wa maabara,” amesema Ndungulu.
Aidha
Ndungulu amesema, uchunguzi wa awali uliofanywa na kamati ulibaini
kuwa watendaji wa manispaa waliingia mikataba mibovu isiyokuwa na tija
na kuisababishia manispaa hasara ya kupoteza mapato sambamba na kulipa
fidia ambazo ni batili, baadhi ya watendaji kushiriki katika ubadhilifu
wa uuzwaji wa mali za manispaa bila kufuata utaratibu, ukodishaji wa
jengo la KIGODEKO bila kufuata sheria.
Ndungulu
amesema, baada ya kubainika kwa tuhuma hizo ofisi ya mkoa imeamua
kuwasimamisha kazi watumishi hao ili kupisha uchunguzi zaidi kuhusu
tuhuma hizo ambapo uchunguzi zaidi ukikamilika hatua zingine za kisheria
zitafanyika.
Aliwataja
majina watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Wilfred Mwita (Mkuu wa
Idara ya Mipango Manispaa), Emmanuel Mkwe (Mwanaseheria wa Manispaa),
Mhandisi Boniface William (Mhandisi wa Manispaa), Mussa Igugu (Mkuu wa
Kitengo cha Biashara), Elimboto Zacharia (Mkaguzi wa Ndani wa Manispaa),
Leonard Nzirailunde (Afisa Misitu), Shida Thadei (Afisa Ugavi), Gwawili
Mkoka (Mhasibu wa Manispaa) na Omary Hassan (Fundi Mkuu wa Magari).
Hata
hivyo Ndungulu alisema, Ofisi ya Mkoa imemuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri Mhandisi, Boniface Nyambele, kusimamia urejeshwaji wa mali
za Manispaa zilizouzwa bila kufuata sheria na taratibu.
“Pia
tumewaagiza jeshi la polisi na TAKUKURU kuchunguza tuhuma hizo kama
kuna mianya ya rushwa ili kama kuwa watu walihusika katika utoaji wa
rushwa basi nao washughulikiwe kwa mujibu wa sheria,” alisema Ndunguru.
0 comments:
Post a Comment