Baadhi ya raia wema na mmiliki wa duka Faustine Samweli wakishirikiana kuokoa mali ndani ya duka lililokuwa linaungua moto.
Freezer linalodhaniwa ndio chanzo cha moto huo.
Askari wa kikosi cha zimamoto manispaa ya Kigoma Ujiji wakiwa kwenye harakati za kuzima moto huo.
Wananchi wakishanga juhudi za polisi na zimamoto wakikabiliana na moto huo.
Na. Pardon Mbwate na Anamaria Masika wa Jeshi la Polisi Kigoma
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limefanikiwa kuzuia na kuokoa mali na kudhiti moto kwa kushirikiana na askari zima Moto wa kikosi cha zimamoto Halmashauri ya Kigoma Ujiji na Kikosi cha zimamoto viwanja vya Ndege na baadhi ya vitu vimeokolewa na vingine kuungua bado thamani yake haijajulikana.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya amemtaja mmiliki wa duka hilo kuwa ni Faustine Samweli 39, Mfanyabiashara wa Lumumba Road chumba NO.16 kiliungua moto.
Kaimu Kamanda amesema kuwa Chanzo cha moto huo ni Freezer iliyokuwa imeachwa ikiwaka usiku mzima bila kuzimwa hivyo kusababisha chanzo cha moto huo.
Kamanda huyo amesema kuwa Thamani halisi ya mali iliyoteketea bado haijajulikana na uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.
Hata hivyo kamanda kihenya amewataka wafanya biashara wa eneo hilo kuhakikisha usalama wa mali zao kabla na baada ya kufanya shughuli zao kuwa waangalifu wakati wa ufungaji wa maduka yao ili kuzuia tukio la aina hiyo.
0 comments:
Post a Comment