Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM, UVCCM Bw. Martin Shigela akishiriki
katika kupalilia shamba la Karanga katika kijiji cha Nkungwe Tarafa ya
Mabembe Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembelea na kujionea shughuli
mbalimbali na kukagua miradi inayotekelezwa na wananchi kwa pamoja na
Serikali jana.
Sekretarieti ya CCM ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman
Kinana iko mkoani Kigoma kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha
Mapinduzi na sherehe za miaka 36 ya chama hicho zinazotarajiwa kufanyika
Februari 3 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo, kulia ni Bi Fatma
mmiliki wa na kushoto ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Kigoma Vijijini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akikabidhiwa zawadi
ya mihogo na Bi Asha Ibrahim mara baada ya kutembelea shamba lake jana, .
Kijiji hicho cha Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha muhogo bra
katika mkoa wa Kigoma.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akiongozana na
Bw.Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini mbele yake
wakati akikagua shughuli za ukulima wa kisasa katika kijiji cha Nkungwe Kigoma
Vijijini, Kijiji hicho cha Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha muhogo bra
katika mkoa wa Kigoma.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimsaidia
Bi. Asha Ibrahim kufukia mbegu ya Viazi, huku viongozi mbalimbali wa CCM wilaya
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimkabidhi
zawadi ya shilingi elfu 10,000 mtoto Rehema huku mama yake akimsaidia wakati
alipotembelea na kujionea shughuli za kilimo katika kijiji cha Nkungwe jana
Viongozi mbalimbali wakikagua kivuko cha Mto Ruchi katika kijiji cha
Nkungwe jana.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akivuka katika
kivuko cha Mto Ruchi kwa kutumia Baiskeli huku akiwa ameonozana na viongozi
mbalimbali wa CCM wilaya ya Kigoma Vijijini pamoja na watendajiwa kijiji hicho
jana inaelezwa kwamba watu wengi walipotea maisha kwa kuliwa na Mamba kabla
ya kujengwa kivuko hiki.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimenya
muhogo
ili kutafuna kidogo mara baada ya kununua kwa mmoja wa wakulima Kijiji cha
Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha Muhogo mkoani Kigoma
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akiagiza
jambo kwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kigoma Bw Peter Msanjila wakati
alipotembelea kata ya Mwanduga jana kulia ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Kigoma Vijijini
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akizungumza na
wanafunzi wa shule ya msingi ya Kabanda katika kijiji cha Chabwimba jana
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akisalimiana na
wananchi mara baada ya kuwasili katika Kata ya Mabembe.
Wananchi wa kijiji cha Mabembe wakimsikiliza mwenyekiti wa UVCCM
katika Kata ya Mabembe kwenye mkutano wa ndani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akicheza na
msanii chipukizi wa kijiji cha Mabembe ambaye ni mlemavu wakati alipotembelea
na katika Kata ya Mabembe
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kata ya Mwanduga
Kigoma vijijini jana
Mjumbe wa NEC CCM kupitia Wilaya ya Uvinza Asha Baraka akiwa katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mwanduga Kigoma jana kulia ni
Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Kigoma Vijijini na katikati ni Peter Msanjila Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kigoma.
Martin Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akihutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika jana kwenye kata ya Mwanduga Wilaya ya Kigoma vijijini
Matin Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akipata maeleo kutoka kwa
Khamis Bitese Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembele
na kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi ya Kabanda.
Martin Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akipata maeleo kutoka kwa
Khamis Bitese Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembele
na kukagua ujenzi wa numba za walimu katika shule ya msingi ya Kabanda.
Huu ndiyo mto Ruchi unaotenganisha kijiji cha Nkungwe na mashamba ya
wanakijiji hao uliosababisha mauaji ya wananchi kadhaa kutoka na kuliwa na
Mamba kabla ya kujengwa kwa kivuko hicho.
0 comments:
Post a Comment