Home » » Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana Ashiriki Kwenye Ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Kijiji cha Bunyambo Wilayani Kibondo na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro Azindua Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Kigoma

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana Ashiriki Kwenye Ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Kijiji cha Bunyambo Wilayani Kibondo na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro Azindua Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Kigoma



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki
ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Bunyambo Wilayani Kibondo,
Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36
ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja
wa Lake tanganyika mjini Kigoma. Wengine ni baadhi ya viongozi na
wananchi aliofuatana nao kwenye msafara wake.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki
ujenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Bunyambo wilayani Kibondo,
Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36
ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja
wa Lake tanganyika mjini Kigoma. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Kaborou.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akishiriki
ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya sekondari Kumwambo, Wilayani
Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya
miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013
kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini Kigoma. Wengine ni badhi ya
viongozi waliokuwa kwenye msafara wake, Mwenyekiti wa  Wazazi Tanzania,
Abdallah Bulembo (aliyebeba tofali) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma,
Dk. Amani Kaborou.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na msafawa
wake, wakinunua miwa njiani baada ya kukutana na muuzaji wa miwa hiyo,
wakati wakitembea kwa mguu zaidi ya kilometa moja kwenda kwenye mkutano
wa hadhara Kijiji cha Bunyambo, baada ya kushiriki shughuli za ujnezi wa
Ofisi ya CCM katika kijiji hicho, Wilayani Kibondo, Januari 31, 2013,
ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo
kilele chake kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake
tanganyika mjini Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na
wanafunzi wa shule ya sekondari Kumwambo, Wilayani Kibondo, Januari 31,
2013, baada ya kushiriki ujenzi wa chumba cha darasa, ikiwa ni sehemu ya
sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake
kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini
Kigoma.
Baadhi ya wazee, watendaji na wajumbe wa mashina wakimsikiliza
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipozungumza
nao kwenye ukumbi wa Maendeleo wa Kibondo, Januari 31, 2013, ikiwa ni
sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM ambayo kilele chake
kitafanyika  Februari 3, 2013 kwenye Uwanja wa Lake tanganyika mjini
Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akirusha mpira golini ikiwa ni ishara
ya uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum
kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha
Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa
Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wachezaji wa timu za
Mwandiga Queens,Lake Tanganyika na Mwananchi muda mfupi kabla ya
kufanyika wakwa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete
(Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha
Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa
Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akizungumza na wachezaji wa timu ya
Shule ya Sekondari ya Mwananchi  wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya
mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya
Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe
3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.
 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akisalimiana na mmoja wa wachezaji
wa timu ya Mwandiga Queens wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa
mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya
Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye
Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa