Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Bi Hadija Nyembo amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kuacha tofauti zao za kisiasa na badala yake kuunganisha nguvu katika kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo mpya iliyozunduliwa hivi karibuni.
Akizungumza katika kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo muda mfupi baada ya uchaguzi wa viongozi wa halamasahauri hiyo Bi Nyembo amesema madiwani hao wanaotokana na vyama vitatu tofauti vya siasa vya CCM, NNCCR MAGEUZI NA CHADEMA wanalo jukumu kubwa la kuwatumika na kuwaletea maendeleo wananchi kama yalivyo malengo ya kuchaguliwa kwao.
Amesema kutokea kwa migogoro na mivutano yaweza kuwa ni vikwazo vya kufikia maendeleo na hivyo madiwani hao wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa
Katika uchaguzi wa baraza la madiwani hao Diwani wa kata ya kandaga katika wilaya hiyo Fransins kumbo kupitia chama cha NNCR Mageuzi amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza wa halmashauri hiyo huku Lucas kanoni Diwani wa kata ya.kazuramimba kupitia chama cha Demorasia CHADEMA akiwa ni makumu mwenyekiti
0 comments:
Post a Comment