Home » » Dk. Slaa: Mawaziri mzigo watoswe

Dk. Slaa: Mawaziri mzigo watoswe

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewang'ang'ania mawaziri ambao wameelezwa kuwa ni mzigo ndani ya serikali kwa kukitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusimamia suala hilo ili kuhakikisha wanatimuliwa.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbroad Slaa,alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Muhange wilayani Kakonko mkoani Kigoma ikiwa ni mfululizo wa ziara yake ya siku 20 kutembelea mikoa ya Kanda ya Magharibi.

“Mbunge wenu (Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Christopher Chiza), ni miongoni mwa mawaziri ambao wameambiwa na CCM waondoke, kama mtu ameshindwa anafukuzwa kazi,tunawalipa pesa lakini hawafanyi kazi ipasavyo,” alisema.

Chiza ni Mbunge wa Buyungu katika wilaya mpya ya Kakonko.Mawaziri wengine walioambiwa na CCM kuwa ni mzigo na wanatarajia kuitwa kujieleza mbele ya Kamati Kuu ya CCM. Wengine ni wake, Adamu Malima; Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

Dk.Slaa alisema ni aibu kwa CCM kubembeleza mawaziri mzigo kwani kama wameshindwa kazi watimuliwe, hiki ni kielelezo kuwa serikali nzima imeshindwa kazi.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa