Home » » MTAALAMU AONYA KUHUSU UCHIMBAJI URANI

MTAALAMU AONYA KUHUSU UCHIMBAJI URANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwanasheria Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na mtafiti wa masuala ya madini,Flaviana Charles.
Watanzania wametakiwa kufuata ushauri wa kitaalam wa wanasayansi kabla ya kuanza uchimbaji wa madini ya urani na kuachana na propaganda za kisiasa nchini.
Wito huo ulitolewa na Mwanasheria Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na mtafiti wa masuala ya madini, Flaviana Charles, wakati akizungumza katika mjadala wa wazi kuhusu madhara ya uchimbaji madini hayo kwa wananchi, ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kuwashirikisha wanaharakati ngazi ya jamii (GDSS).

Alisema kabla ya kuanza mchakato huo maandalizi ya kuhifadhi mazingira kunahitajika ambayo hayataleta madhara kwa kizazi sasa na kijacho.

“Serikali inasema tutaweza kupata ajira za kutosha, umeme wa uhakika wa kutumia madini hayo, tukumbuke madini haya yana mionzi ya hatari kwa afya zetu na vilevile kunahitajika miundombinu ya kutosha hasa ya maji,” alisema Charles na kuongeza kuwa rasilimali zilizopo nchini zingeweza kutosha kuleta ajira, umeme wa uhakika pamoja na kuwainua wananchi na uchumi wao.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa