Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea msaada wa chakula kwa ajili ya
Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma chenye thamani ya Dola ya
Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3 Bilioni, ambazo zimetolewa na Serikali
ya Japan. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na Mkurugenzi
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan. Waziri
Chikawe alipokea msaada huo na kumkabidhi Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa WFP, Regan,
Bandari ya Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akipokea galoni ya mafuta
ya kula kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto) ikiwa ni
ishara ya makabidhiano ya chakula cha msaada kwa ajili ya Wakimbizi
kilichotolewa na Serikali ya Japan. Kulia ni Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Shirika
la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan akipokea msaada huo kutoka kwa Waziri
Chikawe ambao una thamani ya Dola za Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3
bilioni katika tukio la makabidhiano lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimshukuru Balozi wa
Japan nchini, Masaki Okada (kushoto) kwa msaada wa chakula wenye thamani ya
Dola za Marekani 1.4 milioni ambao ni sawa na Shilingi 2.3 Bilioni ambao
Serikali yake imetoa kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani
Kigoma. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard
Regan ambaye alikabidhiwa msaada huo baada ya Waziri Chikawe kuupokea katika
sherehe fupi ya makabidhiano iliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO
CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment