Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
IDARA
ya Uhamiaji mkoa wa Kigoma imeelezwa wasiwasi wake wa nchi kuingia
kwenye mtego wa kuchagua viongozi wasio raia kutokana na kuwepo madai ya
viongozi wanaowahifadhi wahamiaji haramu na kuwaajiri.
Ofisa Uhamiaji wa mkoa, Ambrose Mwanguku aliyasema hayo wakati
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea raia 14 waliomaliza
kifungo cha mwaka mmoja gerezani kabla ya kurudishwa nchini kwao.
Alisema katika utendaji wa kazi zao, wamekuwa wakipata taabu kutoka
kwa wananchi vijijini hasa viongozi wa vijiji ambao wamekuwa wakiwatumia
raia hao wageni katika shuguli za uzalishaji mali hasa kilimo na uvuvi.
Mwanguku alisema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia mbinu
mbalimbali za kuhifadhi na kuwatumia raia wa kigeni bila ya kufuata
taratibu na idara yake imekuwa ikipata taarifa juu ya kuwepo watu hao.
”Hali hii ya kuendelea kuishi katika jamii na raia wasio Watanzania
inaweza hata kutupelekea kupata viongozi ambao si Watanzania, sasa kazi
ya kutoa vitambulisho vya Taifa inakuja, kuna baadhi wanaweza kupata
nafasi na kuandikishwa jambo ambalo ni hatari kwetu,”alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment