Home » » AIRTEL, UNESCO WAZINDUA REDIO UVINZA

AIRTEL, UNESCO WAZINDUA REDIO UVINZA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa redio hiyo uliofanyika mkoani hapa hivi karibuni, Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi alisema wanafurahi kuwa mstari wa mbele kuleta mapinduzi ya mawasiliano kwa kushirikiana na UNESCO kupitia mradi wa redio jamii na kuwawezesha wakazi wa Uvinza kupata mawasiliano.
“Radio jamii tunayozindua leo itawawezesha wakazi zaidi ya 400,000 wanaoishi Uvinza na vijiji vya jirani kupata habari na taarifa za yanayotokea Tanzania na duniani kwa ujumla,” alisema Hawa.
Msimamizi wa Mradi wa Habari na Mawasiliano wa UNESCO Dar es Salaam, Yusuph Al Amin alisema ushirikiano wao na Airtel umefanikiwa na sasa wamewafikia watanzania zaidi ya milioni 16 kupitia redio jamii zilizopo kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Redio, Nuru Kalufya aliwaongeza Airtel na UNESCO kwa msaada huo.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa