Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
.Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred akizindua ujenzi wa bweni la Albino Buhangija mkoani Shinyanga.
Miss
Tanzania 2012, Brigite Alfred akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi
yake ya BAF ambayo kwa kushirikiana na Junior Achievement (JA) huku
lengo kuu likiwa ni kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa albino Tanzania
nzima. Kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye ulemavu wa
ngozi (albino), Mohamed Chanzi.
Miss
Tanzania 2012, Brigite Alfred akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Albino mara baada ya kuzindua mafunzo ya Ujasiriamali Makumbusho ya
Taifa.
……………
Taasisi
ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) kwa
kushirikiana na Taasisi ya Junior Achievement (JA) imeendeleza zoezi la
kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa wajamii ya watu wenye albino
nchini.Mafunzo hayo ya wiki mbili yalifunguliwa na mkuu wa mkoa wa
Kigoma ambapo jumla ya albino 20 walifaidika na mafunzo hayo
yaliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma, kanali mstaafu Issa Machibya.
Mbali ya watu wenye albino, washiriki wengine katika mafunzo hayo
walikuwa wanawake na vijana.
Machibya
alitoa wito kwa taaisis nyingine kuiga mfano taasisi ya Brigitte na
Junior Achievements ambayo mpaka sasa imetoa mafunzo kama hayo kwa
vijana na akina mama 25,000.Mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa mafunzo ya
ujasiliamari ni muhimu kwa kila mtu na kupongeza juhudi za mrembo huyo
ambaye mpaka sasa ametoa mafunzo kwa watu wenye albino 70. Kati ya hao
70, albino 50 walipata mafunzo jijini Dar es Salaam.
“Haya
ndiyo mambo muhimu ya kuigwa kwa jamii, taasisi ya Brigite imetoa elimu
ambayo itawawezesha wahitimu kufanyakazi ya ujasiriamali na kujipatia
kipato kwa jasho lako, nawapongeza sana na taasisi nyingine zifuate
nyayo,” alisema Mashibya.Mratibu wa mafunzo hayo, Stanley Mosha alisema
kuwa kwa kupitia BAF kwa sasa unaende vizuri na lengo lao ni kutoa
mafunzo kwa watu wenye albino kila mkoa na wamepanga kutoa mafunzo kwa
albino 300 nchi nzima kwa mwaka 2015.
Mosha
alisema kuwa lengo lao mafunzo hayo ni kuwawezesha kiuchumi
vikundimbalimbali hususani vijana na wakinamama. Alisema kuwa hatua hiyo
imetokana na mafanikio ya Brigitte katika mashindano ya urembo ya Dunia
ya mwaka 2013 nchini Indonesia na kushika nafasi ya tatu kupitia taji
la mrembo mwenye malengo baada ya kuonyesha dunia jitihada zake za
kusaidia watu wenye ualbino nchini Tanzania.
Alisema
kuwa kuanzia hapo, Brigitte amekuwa Balozi wa watu kwa watu wenye
ualbino Tanzania na kufanya shughuli mbalimbali za kuwasaidia mfano
ujenzi wa bweni la kisasa lenye uwezo wa kuchukua idadi ya watoto 60, na
uboreshaji mazingira kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga.
“Nimefuraishwa
na Mwitikio na ushirikiano walioonyesha kwa kutambua na kukubali
kuliingiza kundi hili na kuweza kuungana na makundi mengine ya vijana
katika program za ujasiriamali. Kulitambua na kulijumuisha kundi hili
katika kuwajengea uwezo ni hatua kubwa inayowezesha kupanua wigo na
juhudi za kuwezesha makundi ya vijana na wakinamama kiuchumi na tunaomba
wadau wengine waungane nasi katika hili,” alisema Mosha.
Kwa
upande wake, Brigitte alisema kuwa ataendeleza mpango huo hapa nchini
na anaamini atafikia lengo lake. “Nashukuru Junior Achievement kwa
kuniunga mkono katika mpango huu ambao kwa sasa unapata mafanikio
makubwa, naomba kuungwa mkono kwani jukumu hili ni la watanzania wote,”
alisema Brigitte.
0 comments:
Post a Comment