Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu
tawala wa Mkoa wa Kigoma akitoa heshima zake za mwisho kwa askari wa
JKT wa kikosi cha 821 Bulombora Kigoma waliofariki jana kwa ajali ya
gati.
Askari
wa majeshi yote wakishirikuana kuweka miili ya wenzao katika eneo la
kutilea heshima za mwisho waliofariki jana kwa ajali ya gari.
Na Editha Karlo wa
Globu ya Jamii, Kigoma
MIILI
saba ya vijana wa jeshi la kujenga Taifa(JKT) kikosi cha 821
Bulombora waliofariki dunia jana kwa ajali ya gari wameagwa leo na
kusafirishwa makwao kwaajili ya mazishi.
Akiongea
na waombolezaji waliofika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa
kigoma(Maweni)kwaajili ya kuaga miili ya marehemu Mkuu wa vikosi vya
Kigoma, Kanali Msuya alisema jeshi limepoteza nguvu kazi ya Taifa .
Alisema
mpaka sasa taratibu zote za kusafirisha miili hiyo zimeshakamilika
miili yote itaondoka kwa usafiri wa magari hadi mwanza na kesho
watasafirishwa na ndege ya jeshi kwenda dar es salaam kwaajili ya
kupelekwa kwenye mikoa yao kwa maziko.
Kanali
msuya aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni MT 54407 SGT Ally
Kambangwa mkazi wa mtwara,MT 108151 PTE Abeli Maisha mkazi morogoro,SM
Eugini Bitati mkazi wa kibondo.
Wengine ni AH 7190 SM Saidi Sadara mkazi wa Shinyanga,RES Bakari Kibaya mkazi wa Tanga,RES Fredrick Kahemela mkazi wa arusha.
Msuya
aliwataja majeruhi pia majina yao kuwa ni Benadicto Ndokeye,Raphael
Yohana,Athanas Emanuel,Abuu Nzoge,Abubakari peter,Abubakari Msubi na
Denis Manyanya.
Wengine
ni Edward Nyanda,Elias Magessa,Gofrey Maliki,King Kasefu,Kamilius
Agida,Stive Denis,Saidi Omary,Saidi Zuberi,Shabaani Zakari,victor
John,Jackson Nyarubu na Mohamed Nyimbo
Naye
katibu tawala wa Mkoa wa kigoma eng.John Ndunguru alisema kuwa serekali
ya mkoa imepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya askari hao saba na
watashirukuana na wafiwa bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.
"Serekali
ya mkoa ina masikitiko makubwa kwa kupokea habari hizi za kuondokewa na
askari wetu tutashikiriana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu"alisema
Ndunguru.
0 comments:
Post a Comment