Na Jacquiline Mrisho - Kigoma
Buluku
aliongeza kuwa hadi sasa kuna jumla ya mashirika yasiyo ya kiserikali
17 yanayoshirikiana na Serikali kuhudumia Kambi hiyo ambapo huduma zote
zinaongozwa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) hivyo,
kazi kubwa ya Serikali ni kusimamia na kuhakikisha mashirika yote
yanatoa huduma zinazofaa kwa wakimbizi hao.
Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imewasaidia jumla ya wakimbizi
55,320 kutoka Burundi kwa kuwapa makazi na kuhakikisha ulinzi wa maisha
yao katika Kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo, Mkoa wa Kigoma.
Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Kambi hiyo,
Peter Buluku wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii juu ya hali
halisi ya maisha ya wakimbizi wanaoishi katika kambi hiyo pamoja na
misaada inayotolewa na Serikali pamoja na Mashirika yasiyo ya
kiserikali.
Buluku
amesema kuwa wakimbizi hao ni raia wa Burundi ambao wamekimbia nchini
kwao kutokana na vurugu zilizojitokeza mwezi Aprili mwaka 2015 ambazo
zilisababisha raia hao kukimbilia nchi za jirani ikiwemo Tanzania.
“Sisi
kama Serikali tunasaidia wakimbizi kwa kuwapa ardhi kwa ajili ya
makazi, kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wakimbizi,kupokea, kusajili na
kutunza kumbukumbu za wakimbizi pamoja na kuunganisha familia za wakimbizi zilizopoteana wakati wa machafuko nchini mwao”, alisema Buluku.
Alifafanua
kuwa kazi ya kutoa huduma za kijamii zikiwemo za Afya, Chakula, ujenzi
wa nyumba, masoko,vyuo vya ufundi na miundombinu, Maji, huduma za haki
za watoto na wazee wasiojiweza, elimu pamoja na huduma za kutoa misaada
ya kisheria zinafanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyojitolea
kuwasaidia wakimbizi hao.
Mkuu
huyo wa Kambi ametaja changamoto kubwa inayoikabili kambi hiyo kuwa ni
upungufu wa rasilimali fedha kwa mashirika ambayo hali hiyo husababisha baadhi ya shughuli za kuiwezesha kambi hiyo kutofanikiwa.
mwisho
0 comments:
Post a Comment