Mkuu
wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya
Mahale,Mhifadhi ,Romanus Mkonda akizungumza na kina mama wanaofanya kazi
ya kuponda mawe mwambao mwa ziwa Tanganyika kwa lengo la kupata kokoto
ambazo TANAPA imekua ikinunua kwao kwa ajili ya ujenzi wa mioundo mbinu.
Kina
mama katika kijiji cha Buhingu wilayni Uvinza mkoani Katavi wakipasua
Mawe kwa ajili ya kuponda ili kupata Kokoto ambazo zimekua zikinunuliwa
na Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano na Hifadhi ya Taifa
ya Mahale inayopakana na kijiji hicho.
Katibu
wa waponda Kokoto katika kijiji cha Buhingu Neema Jackson akisoma
risala mbele ya viongozi wa Hifadhi Taifa ya Milima ya Mahale na TANAPA
walioongozana na wanahabri kutembelea kina mama hao.
Kazi
ya upasuaji wa Mawe katika kijiji vcha Buhingu kimekuwa pia kikifanywa
na kina mama ambao umri wao umeenda ili kusaidia familia zao.
Sehemu
ya kokoto zilizokwisha patikana ambazo hata hivyo kina mama hao
wamelalamikia bei ndogo wanayolipa Makandarasi wanao pata zabuni ya
ujenzi wa miundo mbinu ambapo wamekua wakilipwa sh 500 kwa ndoo tofauti
na bei ya Sh 1000 kwa ndoo inayo lipwa na TANAPA pindi inapohitaji
malighafi hiyo.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal
Shelutete akizungumza na kina mama hao mara baada ya kusilikiliza
changamoto za kina mama hao.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal
Shelutete akimueleza jambo na Katibu wa waponda kokoto Neema Jackson
akitizama namna ya kushauri makandarasi wanaopewa dhabuni ya ujenzi na
TANAPA kuhakikisha wanatumia malighafi za kina mama hao.
Menea
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pscal Shelutete
akikabidhi kiasi cha Sh 100000 kwa katibu wa kina mama hao mara baada ya
kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya Watoto wanaoshiriki kusaidia wazazi wao katika shughuli ya upondaji kokoto katika kijiji hicho.
Kina
mama wanao ponda kokoto wakifurahia na Meneja Mawasiliano wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascla Sheluetete mara baada ya kutoa fedha
kwa kina mama hao.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kigoma.
0 comments:
Post a Comment