Home » » DC KASULU AKERWA NA WAFUGAJI WANAOHARIBU MSITU WA KAGERANKANDA

DC KASULU AKERWA NA WAFUGAJI WANAOHARIBU MSITU WA KAGERANKANDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na FK Blog- Kigoma,
MKUU wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi ameeleza kukerwa na tabia ya wakulima na wafugaji wanaovamia hifadhi ya Msitu wa Kagerankanda na kufanya shughuli za ufugaji na kilimo katika msitu huo wenye sifa pekee ya Uoto wa Asili Mkoani Kigoma.

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki katika kikao cha Baraza la madiwani kilichokuwa kikiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa kamati husika  katika kipindi cha Julai-Septemba 2016, ambapo mkuu huyo wa Wilaya alitumia nafasi hiyo kuwaasa madiwani wahamasishe wananchi  wapishe  hifadhi hiyo kabla ya kutumika nguvu ya ziada.

Kanali Mkisi alisema  changamoto ya uvamizi katika msitu huo ni ya muda mrefu na kueleza kusikitiswa na vitendo hivyo kutokana na kuwa vitendo hivyo ni janga kwa kizazi cha kijacho, kutokana na makundi ya wakulima na wafugaji kuendelea kujazana katika msituni huo kwa shughuli za kilimo na ufugaji wakati kuna maeneo makubwa yapo wazi na yana rutuba kwa uzalishaji wa bidhaa zao. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

“mimi ni kanali siendeshi wilaya kiraia ,nataka sheria,kanuni na taratibu zitumike katika kurasimisha makazi si kuvamia misitu ya asili yenye hadhi ya uoto wa asili na mimi niseme ukweli, nashangzwa na baadhi ya viongozi wanalifumbia macho wakati rasilimali inatumiwa hovyo kwa maslahi yenu binafsi”  alisema

Aidha Mkisi alisema, hatojali  zengwe kwa kuwa amechaguliwa na serikali hivyo nitasimamia sheria, kanuni na taratibu husika, na kusema kuwa aliondolewa katika nafasi  yake huku akiwa anasimamia sheria na kanuni hatosita  kuendelea na shughuli nyingine.

Akizungumzia kero ya uvamizi wa hifadhi hiyo Diwani wa kata ya Kagerankanda Ezekieli Mshingo, alikiri wananchi kutumia msitu huo kwa zaidi ya miaka 12 kama kichaka cha wahamiaji haramu,ufichwaji wa silaha haramu za moto pamoja na makundi ya wafugaji na wakulima kuongezeka kila kukicha.

Mshingo alisema uvamizi unatokana na usimamizi mbovu kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini na kitendo cha kuwaondoa makundi hayo katika msitu wa kagerankanda ni changamoto kwa kuwa, wavamizi wengi wanasaidiwa na watu wakubwa  hali inayochangia mauwaji  kila mwaka na kutolea mfano wa  Novemba 3, 2016 kuna mfugaji  mmoja Majigwa Magesa ameuwawa na mwishoni na kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya waharifu.

 Naye  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu vijijini Yohana Mshita alisema taifa lilipofikia linahitaji kiongozi muwazi, mkweli mwenye moyo wa dhati katika  kuondoa kero za wananchi kwa uadilifu  huku akifuata sheria zilizopo lengo lkiwa ni kutimiza malengo yake na kusema kuwa katika utendaji huo  baadhi ya watendaji wa halmashauri za wilaya wamekua na taba ya majungu ya kukwamisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali hivyo kumuomba mkuu huyo kutosikiliza maneno yao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa