Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Umoja
wa Viijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) umesema vijana wanaoendelea
kulalamika bila kufanya kazi, kujituma na kutoa jasho la uchapakazi
watakawia sana kufikia malengo chanya na kujikwamua hatimaye maisha.
Hayo
yameelezwa jana kaimu katibu mkuu shaka Hamdu Shaka alipotembelea
kikundi cha ujasiriamali katika kata ya Mwandiga wilaya ya Kigoma
vijijini Mkoani.
Shaka
alisema hakuna njia mbadala na ya mkato ya kujikwamua kimaisha na hali
ngumu yoyote ya umasikini bila kijana mwenyewe kuamua kujishughulisha na
kuzalisha mali hatimaye kujitegemea.
Aliwasifu
wana kikundi hicho kwa kujikusanya, kupanga mipango na mikakati ya
mradi wa kufyatua matofali, kuzalisha sabuni na kuwa na kikundi cha
Vicoba kwa mtimdo wa kuweka na kukopa pia kununu hisa.
"Vijana
wengi huwa wanawaza, wanapanga na kutaka kutenda hawatendi, kikundi
hiki ni makini na kimeamua kuonyesha kwa vitendo jinsi kilivyopania
kujikwamua na umasikini wa vipato hatimaye kujijenga kiuchumi "Alisema
Shaka .
Shaka
aliwahimiza watendaji wa halmashauri ya Kigoma vijijini kuona haja ya
kukipa umuhimu kikundi hicho kwa kuwapatia wataalam, mitaji na vyanzo
vya fedha.
"Vijana
mnakawia, jiungeni ili kushiriki katika shughuli za ujasiriamli kwa
lengo la kuacha utegemezi badala yake mjiajiri na kujitegemea kiuchumi
kama kikundi cha "Alisema
Kaimu
Katibu Mkuu pia alizindua kazi za uchimbaji wa mitaro kwa akili ya
usambazaji wa maji safi na salama katika kata ya kalinzi na kutazama
maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tangi la maji hatimaye akazumgumza na
wanachama katika kikao cha ndani katika kata Mgaraganza mkoani hapa
Kwa
upande wake Mbunge wa vijana Mkoa Kigoma Zainab Katimba ameahidi
kukisaidia kikundi hicho kwa kuwapatia vyerehani vitano ili kuongeza
mradi mwingine wa ushonaji kwa kina dada wa kikundi hicho.
Aliwaeleza
vijana hao waendelee na shime hiyo ya kujitolea na kutumia nguvu zao
ili kufikia malengo yao ya kujijenga kiuchumi na kupata maisha bora.
"Ingelikuwa
vijana wote kigoma na Tanzania wanapitisha maamuzi mazito kama kikundi
hiki, nchi yetu isingekuwa na vijana wanaolalamika, wanaosaka ajira au
kulalamikia umasikini "Alisema Zainab.
Hata
hivyo Mbunge huyo alisema atafanya kila linalowezekana kuhakikisha
vijana hao halmshauri ya Kigoma vijijini inawafuatilia na kuwatazama kwa
macho mawili makoni vijana hao.
0 comments:
Post a Comment