Home » » VIONGOZI WOTE WALIOHUSIKA KUPOKEA MIFUGO PAMOJA NA WAFUGAJI KUTOKA NJE YA NCHI WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA-WAZIRI MPINA

VIONGOZI WOTE WALIOHUSIKA KUPOKEA MIFUGO PAMOJA NA WAFUGAJI KUTOKA NJE YA NCHI WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA-WAZIRI MPINA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza jambo na
kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, kanali Marco Gaguti mara baada ya ukamataji wa Ng'ombe Wilayani kasulu Mkoani Kigoma
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza jambo na
kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe wakitafakari jambo kwa pamoja.

Na Rhoda Ezekiel Kigoama.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, ameagiza Viongozi wote waliohusika kupokea mifugo Pamoja na wafugaji kutoka Nje ya nchi kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya uchunguzi kukamilika ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji watakao gundulika walijihusisha na suala hiloni kinyume na maadili ya utumishi wa uuma.

Hata hivyo waziri huyo aliongoza zoezi la ukamataji wa Ng'ombe zilizo ingizwa nchini kinyume na utaratibu jumla ya Ng'ombe 1580 wanashikiliwa na kuagiza Ng'ombe hizo zitaifishwe na kupigwa mnada baada ya uchunguzi kukamilika na kuhakikisha ifikapo Novemba 10 mwaka huu Mifugo yote iliyoingia kinyume na utaratibu ziwe zimeondolewa kabisa.

Akizungumza juzi mara baada ya ukamataji wa Ng'ombe Wilayani kasulu Mkoani Kigoma, Mpina alisema viongozi walioshiriki kupokea mifugo kutoka Nje ya Nchi viongozi wa aina hiyo washughulikiwe kisheria anaejihusisha na suala la kuingiza mifugo hiyo kama itathibitika hawawezi kuwa na viongozi wanowahifadhi wahalifu wanaoingia Nchini bila kujali masilahi ya nchi na Ng'ombe zimekuwa kero kwa kuharibu Mashamba ya wananchi na Katika maeneo mengi ya hifadhi yameharibiwa sana na Wavamizi hao.

Alisema mpaka sasa mifugo yote iliyokamatwa kwa Nchi nzima ni mifugo 9500 na mifugo hiyo itatakiwa kutaifishwa baada ya Wanasheria na maafisa uhamiaji kuthibitisha kuwa iliingia kinyume cha sheria ilikuifanyia mnada na kukomesha wavamizi wote wanaoingia kinyume na utaratibu na kuharibu misitu na kuwa kichocheo cha migogoro ya wakulima na Wafugaji katika Maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, kanali Marco Gaguti alisema katika msako walioufanya wilayani humo wamefanikiwa kukamata Ng'ombe 1580 na kwamba mpaka sasa wanaendelea na oparesheni ya kusaka mifugo hiyo ilikuhakikisha ifikapo novemba10 mifugo hiyo iweimekwisha ondoka na kuhakikisha klhakuna mifugo mingine inayoendelea kuingia kinyume na utaratibu.

Aidha Mkuu huyo alisema ,wapo baadhi ya viongozi walioshirikiana na wafugaji kwa kupokea fedha na kuruhusu mifugo hiyo iendelee kuishi Nchini bila utaratibu, uchunguzi unaendelea kuwabaini na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakao bainika na upelelezi unaendelea kufanyika kwa haraka kuhakikisha kuwa wamesafisha maeneo yote ambayo yamevamiwa na Wafugaji kutoka Nje na kuwabaini wale wote walioshirikiana nao.

Hata hivyo aliwaomba Wananchi kuendelea kutoa taarifa endapo kunawafugaji waliingia katika maeneo yao bila utaratibu na kuacha kuwahifadhi ilikuepusha migogoro ya Wafugaji na wakulima kutokana na wafugaji hao kuingilia maeneo ya wakulima.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa