KATIBU Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akishiriki upigaji chapa mifugo katika Kijiji
cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu
wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia
zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka
huu.
KATIBU Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo akiwaeleza na wafugaji wa Kijiji cha Kabanga
Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma umuhimu wa zoezi la kupiga chapa ikiwa ni sehemu
ya timu ya wataalamu wa wizara hiyo iliyoko katika mikoa 26 ya Tanzania bara
kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa mifugo linalotarajiwa kukamilika
Januari 31 mwaka huu.
Na Kumbuka Ndatta,
KASULU
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi(Mifugo)
Dk. Maria Mashingo ameagiza ng’ombe wote wenye umri wa kuanzia miezi sita na
kuendelea kuhakikisha wamepigwa chapa kabla ya kufikia tarehe ya mwisho ya
upigaji chapa Januari 31 mwaka huu, kwani zoezi hilo sio la hiari bali ni la
lazima na linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria.
Dk. Mashingo
ametoa kauli hiyo wakati akishiriki zoezi
la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Kabanga Wilaya ya Kasulu mkoani
Kigoma ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu wa Wizara hiyo iliyoko katika mikoa
26 ya Tanzania bara kufuatia na kusimamia zoezi la upigaji chapa
mifugo linalotarajiwa
kukamilika Januari 31 mwaka huu.
Dk Mashingo
aliwaambia wafugaji hao kutambua kuwa zoezi hilo linasimamiwa kwa
mujibu wa Sheria
ya utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa
mifugo Na. 12 ya
Mwaka
2010 na kuwasititiza kuwa haijulikani Serikali itaamua nini kwa mifugo
itakayokuwa haijapigwa chapa hadi kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa ya
Januari 31 mwaka huu.
Aidha Dk. Mashingo alitumia fursa hiyo
kuwaelimisha wafugaji sehemu maalum ambayo
ng’ombe anapotakiwa kupigwa chapa mwilini mwake ili kutoharibu ngozi
yake inayotegemewa kwa matumizi mengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu
Emanuel Maganga amesema zoezi la upigaji chapa linaendelea vizuri na
mwitikio ni mkubwa kutoka kwa wafugaji ambapo jumla ya ng'ombe 93,182
wameshapigwa chapa kati ya ng'ombe 345,469 waliotambuliwa ambao ni sawa na
asilimia 27.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa
Halmashauri ya
Mji wa Kasulu, Fatima Laay amemweleza Katibu mkuu kuwa jumla ya ng'ombe 7,552
kati ya 10,000 wenye umri wa zaidi ya miezi sita na kuendelea tayari
wameshapigwa chapa ambao ni sawa na asilimia 75.52.
Kwa upande wake Mbunge wa Kasulu Mjini,
Daniel Nsanzugwanko alikiri kuwepo tatizo la Ng'ombe kupata vidonda vikubwa
wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo jambo lilochangiwa na wafugaji
kutoelimishwa sehemu sahihi ya kupiga chapa mifugo.
"Mimi ng'ombe wangu bado
hawajapigwa chapa,waliopigwa
chapa walipata vidonda vikubwa kwa hiyo kama wataalam wetu ngazi ya vijiji
wameelimishwa vizuri jinsi ya kupiga chapa basi haina shida nitawapeleka
ng'ombe wangu wakapigwe chapa na kuhamasisha wananchi wengine kuunga mkono
zoezi hili "alisema Nsanzugwanko.
0 comments:
Post a Comment