Home » » KIINI VIFO VINGI VYA WAJAWAZITO CHATAJWA.

KIINI VIFO VINGI VYA WAJAWAZITO CHATAJWA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ELIMU duni ya njia salama za uzazi kwa wajawazito, imekuwa kikwazo na kufanya vifo vya wajawazito na watoto kuendelea.
Meneja wa Shirika la World Lung Foundation mkoa wa Kigoma, Adolf Kaindowa amesema vifo hivyo vinaendelea kuwepo, licha ya kuboreshwa kwa vituo vya kutolea huduma na kujengwa kwa vyumba vya upasuaji katika vituo mbalimbali mkoani Kigoma.
Alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahudumu wa afya katika jamii.
Mafunzo hayo yalihusu utoaji elimu na uhamasishaji jamii kutumia njia salama za uzazi wa mpango. Yalilenga kupunguza vifo vya wajawazito na watoto mkoani Kigoma.
Kaindowa alisema bado wajawazito wengi, wameendelea kujifungulia nyumbani na kwa wakunga wa jadi, badala ya vituo rasmi vya utoaji huduma, hivyo kuchelewa kupatiwa huduma, jambo linalochangia kufanya vifo vya wajawazito na watoto kuendelea.
Alisema sababu kubwa ya kuendelea kwa hali hiyo ni jamii kutotambua umuhimu wa wajawazito kuzalia vituo rasmi vya utoaji huduma na kukimbia gharama za kununua vifaa vinavyotumika wakati wa kujifungua.
Mratibu wa Shirika la Engender- Healh mkoa wa Kigoma, Dk Wilfred Mongo alisema bado akinamama wengi hawana uelewa na elimu sahihi ya njia salama za uzazi wa mpango.
 CHANZO; HABARI LEO.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa