Home » » APIGWA HADI KUFA KWA WIZI WA KUKU HUKO KIGOMA

APIGWA HADI KUFA KWA WIZI WA KUKU HUKO KIGOMA

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi Frasser Kashai

Na Pardon Bwate na Felister Elias, wa Jeshi la Polisi Kigoma
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Kagongwa mkoani Kigoma Patroba Christopher(25), ameuawa kwa kupigwa mawe na marungu na kundi la watu wenye hasira baada ya kukurupushwa akiiba kuku kijijini hapo.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidi Frasser Kashai, amesema kuwa juzi majira ya saa 9.00 usiku, marehemu alienda nyumbani kwa Bi. Hawa Ahmed na kuingia kwenye banda la kufugia kuku ambapo aliiba kuku watano wenye thamani ya shilingi 50,000.
Kamanda Kashai amesema kuwa, wakati marehemu akitoka kutoka kwenye banda hilo Bi. Hawa alisikia kuku wakilia na kishindo cha mtu anayekimbia ambao kuku waliendelea kusikika wakilia akitokomea nao na ndipo alipopiga kelele za mwizi na watu walijitokeza kwa wingi na kuanza kumfukuza marehemu huku wakimshambulia kwa mawe na marungu hadi kufariki dunia.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa