Home » » JESHI LA POLISI MKOANI KIGOMA LAKAMATA SILAHA MBILI ZA KIVITA AINA YA SMG NA RISASI MBILI.

JESHI LA POLISI MKOANI KIGOMA LAKAMATA SILAHA MBILI ZA KIVITA AINA YA SMG NA RISASI MBILI.


Kaimu Kamanda Kihenya Kihenya akiwaonesha waandishi wa Habari Silaha mbili za Kivita aina ya SMG zilizokamatwa katika kitongoji cha Lugongoni kata na tarafa ya Nguruka wilaya ya Kigoma mkoa wa Kigoma.
Ssp Kihenya akiwonesha Waandishi wa Habari risasi mbili ziliyokamatwa pamoja na Silaha hizo.
Waandishi wa habari wakiwa ofisini kwa Kaimu Kamanda SSP Kihenya.
Na.Pardon Mbwate wa Jeshi la Polisi Kigoma.
Jeshi la polisi mkoani Kigoma limendelea na operesheni endelevu ya kupambana na uhalifu na wahalifu katika ambapo jumla ya silaha mbili za kivita aina ya SMG na risasi mbili zimekamatwa maeneo ya Nguruka na Mabamba.
Kaimu Kamanda Kihenya SSP amesema mnamo tarehe 07/04/2012 katika kitongoji cha Lugongoni kata na tarafa ya Nguruka wilaya ya Kigoma mkoa wa Kigoma askari polisi waliwakamata watu wanne  akiwemo Ndolimana Alfred Ndoli (29) ambaye ni Mhutu na mkaazi wa Lutana Kiharu nchini Burundi na Matata Chubwa Ntasamba (36), mkulima mkaazi wa kijiji cha Kitanga wilaya ya Kasulu, Ndegeya Medard (28) mkulima mkaazi wa kijiji cha Kitanga wilaya ya Kasulu mkoa wa kigoma, na Bosco Yohana Gabriel (35) ambaye pia ni Mhutu mkulima na mkaazi wa Kibimba Giharu nchini Burundi wakiwa na silaha ya kivita aina ya SMG No. 56 – 2500509 na magazine mbili, huku magazine moja ikiwa na risasi mbili.
Kaimu Kamanda amesema katika maeneo ya mto Ruguzye kijiji cha Mabamba Wilaya ya Kibondo kufuatia msako dhidi ya uhalifu na wahalifu na wananchi kukubali kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi kupitia falsafa ya polisi jamii na ulinzi shirikishi, silaha moja ya kivita aina ya SMG ambayo haiwezi kusomeka namba kutokana na kuwa na kutu nyingi ilisalimishwa kwa kutupwa porini na mtu/watu wasiojulikana.
Silaha hiyo haikuwa na magazine na mwananchi aliyetoa taarifa za kusalimishwa kwa silaha hiyo ni Alistakas  Ernest (35) mkulima mkaazi wa mabamba.
Wakati huo huo Kaimu Kamanda Kihenya amesema katika Kitongoji cha Mrusi Kasulu mjini wilaya ya Kasulu mkoa wa kigoma Elizabeth Kanyungu (46) mkulima, mkaazi wa Seremala Kitongoji cha Mrusi alijinyonga ndani ya nyumba kwa kutumia kamba ya katani.
Marehemu alitumia nafasi ya familia yake kwenda kanisani kusali ndipo yeye alibaki peke yake nyumbani na kujinyonga hata hivyo chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea.
Aidha Kamanda Kihenya amesema jeshi la polisi linawataka wananchi waache kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua wahalifu kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Wananchi hawana budi kuheshimu mamlaka ya vyombo vya hakijinai.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa