Home » » KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIGOMA AWATAKIA HERI YA PASAKA NJEMA WANANCHI WA MKOA HUO NA KUWATAKA KUWA WAANGALIFU

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIGOMA AWATAKIA HERI YA PASAKA NJEMA WANANCHI WA MKOA HUO NA KUWATAKA KUWA WAANGALIFU

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIGOMA,SSP KIHENYA KIHENYA AKIZUNGUNZA NA ASKARI KATIKA VIWANJA VYA PALEDI.
MKUU WA UPELELEZI MAKOSA YA JINAI MKOA WA KIGOMA,SSP JOSEPHU KONYO AKITOA MAELEKEZO KWA ASKARI WAPYA KUTELEZA WQAJIBU NA SHELIA.
ASKARI WAPYA WAKIPEWA MAELEKEZO YA ULINZI SHILIKISHI.
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Katika kuhakikisha kuwa wananchi wanasheherekea sikukuu ya pasaka katika hali ya amani na utulivu, Jeshi la polisi limepanga mikakati madhubuti ya kupambana na uhalifu na wahalifu katika ngazi zote kuanzia vitongoji, vijiji wilaya na mkoa kwa ujumla tumepata Askari wapya wa kutosha .

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya Katika kipindi chote cha sikukuu ulinzi utaimarishwa katika maeneo yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko ya watu kuanzia katika maeneo ya starehe, sehemu za ibada, aidha wamiliki wenye vyombo vya usafiri wanakumbushwa kuzingatia wajibu wao wa kufuata sheria zote za usalama barabarani.

Kaimu Kamanda amesema kuwa wazazi wanakumbushwa kuhakikisha kuwa watoto wadogo wanakuwa na watu wazima wa kuwaongoza barabarani. kwa wamiliki wa kumbi za starehe wanakumbushwa kuzingatia kuingiza watu katika kumbi za starehe kulingana na idadi ambayo kumbi hizo zinastahili ili kuepuka misongamano ya watu inayoweza kuleta maafa.

Amesema Watoto wadogo wasiruhusiwe kwenye mikusanyiko ya usiku kwa mfano bar, na kumbi za starehe. Wazazi na wananchi kwa ujumla ni muhimu kuzingatia kwani hili ni swala la maadili. sanjari na hayo jeshi la polisi linawataarifu wananchi kwa ujumla kuwa hali ya usalama katika manispaa ya mji wa Kigoma ni shwari kwa sasa.

Kamanda Kihenya amesema hii inatokana na kudhibitiwa kwa matukio ya kujeruhi na unyang’anyi wa kutumia nguvu ambayo yalitokea kati ya tarehe 15,16,17 mwezi march 2012. matukio hayo yamedhibitiwa na tangu wakati huo hakuna tukio la aina hiyo lililotokea. Niwatoe hofu Wananchi kupigwa nondo ni uzushi , wahalifu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa