Home » » WAKUFUNZI CHUO CHA NYUKI TABORA WAFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

WAKUFUNZI CHUO CHA NYUKI TABORA WAFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA





Mwandishi Wetu, Kasulu, Kigoma Yetu


Wakufunzi wanne kutoka katika Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora wako Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma katika ziara ya wiki moja kutembelea na kubaini wadau wa ufugaji nyuki ili kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu ufugaji wa nyuki mkoani humo.

Igunda Selele ambaye ni mmoja mwa wakufunzi hao alisema kuwa ziara hiyo itasaidia kuchanganua maeneo muhimu ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa kutoa msaada wa kitaalamu kwa wadau hao wa ufugaji nyuki kwa maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Alisema mbali na kufanya uchanganuzi huo pia wamelenga kubaini maeneo ya wafugaji nyuki ambayo wataweza kuyatumia kuwapeleka wanafunzi wa chuo chao cha Tabora katika ziara za kimasomo ili kuwaimarishia uwezo na ujuzi wa kufuga nyuki katika maeneo hayo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa