Na Iddi Risasi, Kigoma
UJENZI wa vyumba vya upasuaji katika vituo 12 vya afya mkoani Kigoma, kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na kuokoa watoto wanaozaliwa.
Kauli hiyo ilitolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Leonald Sumbi, wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya afya mkoani humo uliokuwa ukijadili mkakati wa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, uliofanyika kwa ufadhili wa Shirika la World Lung Foundation.
Bila kutoa takwimu kuhusiana na jambo hilo, alisema kuwa ujenzi wa vyumba vya upasuaji umezingatia kuboresha huduma katika maeneo ya mbali na hospitali za mkoa na wilaya, lakini pia katika maeneo ambayo yana miundombinu duni ya usafiri.
Hata hivyo, alisema bado Kigoma unakabiliwa na changamoto kubwa ya kuendelea kuwapo kwa vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutokana na wajawazito wengi kujifungulia nyumbani, ambapo kwa sasa zaidi ya asilimia 42 ya wanawake hao wanajifungulia nyumbani, kutokana na kuchelewa kufikishwa hospitalini wanapopatwa na matatizo wakati wa kujifungua.
Alisema suala la uchache wa watumishi katika sekta ya na miundombinu duni ya usafiri katika maeneo ya mbali vijijini kufika katika maeneo ya utoaji huduma za afya ni miongoni mwa changamoto zinazochangia katika ongezeko la vifo hivyo.
Akichangia kuhusiana na jambo hilo, Naibu Mkurugenzi Mkazi wa World Lung Foundation, Hamed Mohamed, alisema Serikali haina budi kuboresha huduma za afya na kuzipeleka kwa wananchi waliopo hasa katika maeneo ya vijijini yenye miundombinu duni.
Alisema sehemu kubwa ya vifo hivyo vinatokea maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa huduma za dharula pale mjamzito anapopata matatizo, zinakuwa hazipo na inachukua muda mrefu kwa mgonjwa kupata huduma katika hospitali za mkoa na wilaya ambazo ziko mbali na pale alipo.
Alisema Serikali kama waajiri hawana budi kuweka vivutio kwa watumishi wa sekta ya afya kuweza kuja kufanya kazi mkoani Kigoma, kwa kuwa mkoa huo umekuwa na historia ya kuwa nyuma kimaendeleo jambo linalowatia woga watumishi hasa wale wanaotoka vyuoni kukubali kufanya kazi mkoani humo.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment