Na Iddi Risasi, Kigoma
WAKATI watu 16 wanaaminika kufa kutokana na Ebola nchini Uganda, Mkuu wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya, amesema Serikali mkoani humo imejipanga kikamilifu kuhakikisha inadhibiti ugonjwa huo kutoingia mkoani humo.
Akizungumza mjini hapa jana, aliwataka wananchi wa mkoa huo kujihadhari na mikusanyiko isiyo ya lazima, ikiwa ni moja ya njia za kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.
Alisema ametoa tahadhari hiyo kutokana na kuwapo kwa mwingiliano mkubwa wa wananchi wa mkoa huo na Uganda, ambao wamekuwa wakienda nchini humo kwa ajili ya shughuli za kibiashara.
Kutokana na hilo, ametaka tahadhari mbalimbali kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kujua dalili za mtu mwenye ugonjwa huo na kutoa taarifa kwa mamlaka mbalimbali za afya mkoani humo.
Alisema kwa sasa ugonjwa huo unasambaa kwa kasi katika maeneo mbalimbali ya Uganda, ambapo awali ulikuwa mashariki ya Uganda na kwa sasa tayari umeshaingia Kampala.
Alisema kumekuwa na mazoea kwa wananchi wa Kigoma kutembelea Uganda, hasa katika Jiji la Kampala kwa ajili ya biashara na kuwapo kwa mwingiliano baina ya nchi hizi mbili.
Alizitaja dalili za ugonjwa huo kwamba ni pamoja na mgonjwa kutokwa na damu katika matundu (vinyweleo) vya mwili wake, mdomoni, masikioni na puani na mgonjwa anaweza kufa katika kipindi kifupi tangu kupatwa na maambukizi.
Alisema wataalamu wa afya na watendaji wa ngazi mbalimbali wamejipanga katika mipaka ya kuingia mkoani humo na hasa ile ya kutoka nchi za maziwa makuu kuhakikisha hakuna mtu mwenye dalili ya ugonjwa huo anaingia bila kuchukuliwa hatua za kuudhibiti.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment