Mwandishi wetu, Kigoma Yetu
Baraza la waislam wilaya ya kigoma (BAKWATA) na Jumuiya ya kuendeleza Qur’an na Sunna(JUQUSUTA) kigoma, wamelaani tamko la kutaka kumchinja hadharani Shekhe Mkuu wa Tanzania Issa ibn Simba kwani kama anamakosa wayafikishe kwa waziri mkuu ili sheria ichukue mkondo wake.
Kauli hiyo ilitolewa jana Mkoani hapo wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wakati akiwa katika harakati za kupata maoni yao juu ya tamko la wanaharakati wakislam wanaotaka kuthubutu kumchinja kiongozi huyo.
Katibu wa Bakwata wilaya ya Kigoma Khalfan Omari alisema kuwa wanaharakati hao, hawanabudi kufuata sheria ya katiba ya jamuhuri ya Muumgano wa Tanzania kwani aliwekwa madarakani kwa kuchaguliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za dini hiyo na kwa viwango mtambukwa kama wanavielelezo vya makosa wafikishe kwa waziri Mkuu naye atasaidia kufanya tija waitakayo na si kukurupuka.
Kwa upande wake Katibu wa wanafunzi wa chuo cha waislamu Morogoro Bilal Sadick alisema kuwa, kauli hiyo haina tija ya kuwakomboa waislam kiuchumi ila Bakwata Taifa kupitia uongozi wake wanatakiwa kukubali mabadiliko ya kiutawala ili kuwajengea uwezo wa kiuchumi waislamu na waondokane na shutuma zinazowakabili.
Alibainisha kuwa, tangu 1970 tasisi hiyo iwe madarakani haina faida kwa jamii hasa katika Nyanja ya elimu, afya na uchumi ukilinganisha na upande wa madhehebu ya kikristo ambao wamepiga hatua zaidi katika kuwapa huduma jamii kupitia huduma zake za afya na elimu.
Mwenyekiti wa JUQUSUTA HajHussein Hanzulun alisema kuwa, haungi mkono kauli hiyo, na wanachotakiwa kufanya wanaharakati hao ni kufuata sunna za Mtume Muha’mad (S.A.W) kwa kuketi mezani na kuzitafutia fumbuzi changamoto zinazoukabili Uislamu na si kauli za kihuni.
Naye Hanzulun aliongeza kwa kusema kuwa, kufuatia hayo, jamii isiuone uislamu ni dini korofi ila baadhi ya waislamu wasio na maadili mema ya malezi kutokana na makuzi ya familia zao ni chachu ya kuuchafua uislamu uonekane ni dini sumbufu.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment