Na Mwandishi Wetu, Kigoma Yetu
JUMLA ya watahiniwa 47 wa Darasa la wa shule za msingi zilizopo katika manispaa ya kigoma Ujiji wamegundulika kuwa hawajui kusoma, kuhesabu na kuandika.
Hayo yamejili Mkoani hapo wakati wa semina elekezi ya kwa Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa shule na Maofisa Elimu wa Vitengo mbalimbali, ikiwa na tija ya kuyabaini mapungufu yaliyopo katika kitengo cha elimu katika manispaa hiyo.
Afisa Elimu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Shomari Bane, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo huchangiwa na matatizo mbalimbali ingawa amedai yeye ni mara yake ya kwanza kuhudhuria kikao kama hicho kwani ni mgeni mkoani hapo, huku akisisitiza kuwa atayafanyia kazi, ili kupunguza idadi hiyo ya wanafunzi wasiojua lolote darasani.
Kwa upande wake Mwalimu Adolf Stanslaus amlisema kuwa, tatizo hilo ni sugu katika shule zilizopo katika manispaa hiyo, kwani kutokana na walimu wenye dhati ya kazi kutopewa motisha, imekuwa chachu ya kutowafundisha watoto kwa tija ya maslai yao ya baadaye.
Naye Maria Katuku ni mzazi pia mwalimu mstaafu amewanyoshea vidole walimu wa kisasa hawana upendo wala wito wa kufanya kazi hiyo tofauti na enzi zao, hivi sasa walimu waliowengi wanasubiri mwisho wa mwezi wapate mgao wao, baada ya kushindwa kupata kazi wazitakazo.
Aidha Katuku alisema kuwa, zamani mwalimu ni zaidi ya mzazi kwani humfatilia mtotokwa kujua masiha yake na familia yake kwa ujulma,na pale anapogundua shida ya mtoto hutafuta mbinu mbadala ya kufanikisha mwanafunzi anaelewa na hatimaye hujua kusoma,kuhesabu na kuandika.
Ntilampa Robert ni miongoni mwa watahiniwa amesema kuwa, changamoto hiyo inaikabili pande mbili yani mwalimu na mwanafunzi, ingawa amekiri kuwa wanafunzi waliowengi hawana tabia ya kusumbua walimu wao kwa tija ya kueleweshwa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment