Na Mwandishi Wetu, Kigoma Yetu.
MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Mjini Moses Machali amewataka
viongozi watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wawajibishwe kwa
kufikishwa mahakani, kwa kitendo cha kushindwa kudhibiti matumizi ya fedha
2010-2011 ambayo imepelekea kupata hati isiyokidhi kiwango.
Kauli hiyo imetolewa kwenye kikao cha Baraza la
madiwani wakati wakisomewa ripoti ya mkaguzi wa hesabu wa serikali Kigoma
Exaud Nikutusya ambapo alitaka majibu ya hoja tete 27 za hesabu kwa
halmashauri hiyo, na kwamba ripoti ya mkaguzi huyo ilieleza
changamoto nyingi ikiwemo matumizi ya fedha yasiyo na stakabadhi.
Pia ripoti hiyo imeonyesha kuwa halmashauri imeshindwa
kuwawajibisha mawakala wa ukusanyaji wa vyanzo vya mapato na matumizi mabaya ya
fedha hasa kutelekezwa kwa jengo la shule ya sekondari ya Muyobozi likiwa
tayari limekamilika hali iliyosababisha wapate hati ya mashaka ambayo
inakaribiana na hati chafu.
Mh. Machali alisema kuwa, halmashauri hiyo imewanyima
uhuru wa mawazo kwa baadhi ya madiwani ambao wanataka mabadiliko ya kiutendaji
kwa wabadhirifu wa mali za wananchi,hali inayosababisha uzalendo wan chi
kushuka kila siku.hali inayolea mfumo wa kuogopa kusema ukweli penye uozo.
“Udhalimu wa kutafuna fedha za serikali siungani nalo
kabisa, nitawaruka mkija mjengoni siwezi kufunika kombe mwanaharamu apite, miongoni
mwetu wapo wachafu wachukuliwe hatua za kisheria na hatimaye wapelekwe
mahakamani wasisababishe halmashauri ipate hati chafu kwa watu wachache” alisema
Machali.
Aisack Mkemwema aliwashatumu watunza kumbukumbu kwa
kushindwa kutunza risiti za mapato na matumizi ya fedha kwa kitendo hicho
inapelekea kuchakachua majibu kwa makguzi wa (SIG),kwani kipooro cha hoja 27
kati ya 31 zilizojibiwa ni dalili ya udhaifu wa halmashauri hiyo,ikiwa
wao ni wanataaluma walitoka vyuoni iweje washindwe kuambatanisha vithibiti vya
hoja hizo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Wiliam Luturi alidadavua
kuwa,ikiwa mh,Machali atawaruka katika changamoto hiyo na madiwani
kutoshirikiana katika kutolea ufafanuzi wa hoja tete 27 kwa mkaguzi na mdhibiti
wa hesabu za serikali basi ikitokea kunyimwa fedha za ruzuku Serikalini
2012-2013 wasilaumiane,huku akiwanyoshea vidole madiwani waache kumtishia
kumtoa uenyekiti kwani kila mtu anamapungufu yake.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Kalvin Mkonda,alikiri
kupokea changamoto hizo,ingawa zingine ziko nje ya uwezo wake,na washutumiwa wa
hoja hizo 27 hawajahudhuria kikao hicho,hivyo wavute subira hadi hapo madiwani
watakapopewa taarifa ya kikao cha pili cha kuzitafutia ufumbuzi hoja hizo(27)
kabla ya Septemba ,28 kwenye kikao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment