Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
Naibu Waziri Uchukuzi Dr.Charles Tizeba ametoa agizo kwa Mamlaka ya Usimamaizi wa Bandari Tanzania (TPA) wapeleke Wakaguzi wa hesabu wa bandari kwa mwekezaji wa upakuaji wa mizigo tawi la Kigoma (MUWAP) na (MSCL) ikiwa na lengo la kujua utendaji kazi wake.
Agizo hilo limetolewa Mkoani Humo kwenye ziara fupi ya waziri huyo, ili kujua changamoto inayoikabili sekta ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwa njia ya meli, ambapo alibaini mapungufu kadhaa katika Taarifa zao pamoja na miundombinu ya meli na vitendea kazi kupitia taarifa iliyosomwa na meneja wa matawi ambayo katika kipengelele cha mapato na matumizi ya fedha yalikuwa na mapungufu hasa MUWAP hawakubainisha.
Alisema, mamlaka hizo kwa pamoja zimekuwa zikitoa lawama ya uchakavu wa miundombinu ya reli kuwani chachu ya kupata mapato finyu kutokana na wafanyabiashara walio wengi kutumia mitumbwi ya watu wachache wenye asili ya Kibembe na malori wakati hali halisi mizigo iliyojaa haionekani na kwamba wanakabiliwa na ukale badala ya ubunifu wa kuteka soko huria ili kwenda na wakati kulingana na mazingira ya sehemu husika.
Dr.Tizeba alisema kuwa, Mv-Liemba haina sifa ya kukwama njiani pindi inaposafirisha abiria na mizigo, hivyo ikifanyiwa maboresho ya miundombinu ambayo nikuweka viti vya plastiki, mashuka bora, feni (AC) kupunguza uvundo wa hewa chafu na kwamba mito iliyopo ya plastiki ni mateso kwa abiria wao hivyo waongeze ufanisi wa maboresho kushindana na soko.
Aidha alitoa agizo kwa mtaalamu wa uchumi wa bandari abaki na watendaji wa MSCL kuwasaidia namna ya kuweza kumudu soko la ushindani.
Hata hivyo aliongeza kwa kusema kuwa, anapatwa na mashaka ya mazingira ya udokozi wa rasilimali fedha kutokana na mikataba ya wafanyakazi walio wengi ni ya muda mfupi huku wakiwa na dhamana ya kushika fedha za serikali na kumwachia mwekezaji dhamana ya kuitangaza bandari hali inayochochea vibarua kuwa wengi na walio na mikataba ni wafanyakazi ambao wanapaswa kuajiriwa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment